Skip to main content

WALICHOJIBU CHENGE ,NGELEJA NA DK.KAFUMU BAADA YA RIPOTI YA PILI YA RAISI.



              VIGOGO waliotajwa katika ripoti ya pili ya kuchunguza makontena yenye mchanga wa madini (makinikia)  kuisababishia Serikali hasara ya matrilioni ya fedha kupitia sekta ya madini, walipokuwa wakihudumu katika nyadhifa zao serikalini wamevunja ukimya.
Vigogo hao wamezungumzia ripoti hiyo ya pili iliyowasilishwa kwa Rais Dk. John Magufuli Ikulu Dar es Salaam jana, ambapo kamati husika ilichunguza hasara ambayo nchi imepata tangu 1998 usafirishaji wa mchanga wa dhahabu nje ya nchi ulipoanza.

Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM), alipoulizwa maoni yake juu ya kutajwa na kamati hiyo, alisema hataki kuzungumza chochote juu ya ripoti hiyo, huku Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), akisema sheria ya madini ya 2010 ingefuatwa, nchi isingekuwa hapa ilipo.
Kwa upande wake Kamishna wa Madini wa zamani, Dk. Dalaly Kafumu, alisema kwa sasa  hawezi kuzungumza jambo lolote kwa kuwa ni yeye ni mmoja wa watuhumiwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo.
Chenge
Baada ya kutoka kwenye kipindi cha asubuhi cha Bunge ambacho alikuwa akikiendesha, Chenge alipotakiwa kuzungumzia ripoti hiyo, alijibu kwa ufupi.
“Sizungumzi na mtu,” na alipoulizwa kama hata salamu hataki, alisema. “Sizungumzi na mtu mimi,” alisema Change ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Chenge alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kati ya 1972 na 1990, ambapo mwaka 1993 aliteuliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali nafasi ambayo alidumu nayo hadi mwaka 2005.
Dk. Kafumu
MTANZANIA ilimpomtafua Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM), ambaye ametajwa kutaka kuingilia ripoti ya kamati ya kwanza iliyochunguza mchanga huo, alisema hataki kuzungumza chochote kwa sasa ingawa anaamini kila kitu kiko sawa.
“Kwa kuwa nimetajwa kama mtuhumiwa, sitaki kusema kitu kwa sasa kwa sababu hili ni sawa na jambo lililo mahakamani tu kwa kuwa wamesema tutahojiwa, lakini kila kitu kiko sawa,” alisema Dk. Kafumu.
Alipoulizwa kama ni kweli alikutana na Profesa Abdulkarim Mruma, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya kwanza na ni nini walichozungumza, Dk. Kafumu alisema. “Nimeshasema no comment (sina la kusema ),” alisema Dk. Kafumu.
Dk. Kafumu ni moja ya watumishi waliohudumu ndani ya Wizara ya Nishati na Madini ambapo alifanyakazi kazi ndani ya wizara hiyo kuanzia mwaka 1983 hadi 2011, alipoacha na kwenda kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa marudio wa Igunga, baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Rostam Aziz.
Taarifa zilizopo kwenye tovuti ya Bunge zinaonesha, mwaka 1983 mpaka 1987, Dk. Kafumu alikuwa mtaalamu wa miamba na madini wa wizara hiyo, mwaka 1987 mpaka 1992, mkufunzi na mtafiti wa madini, mwaka 1992 mpaka 2002 akawa mtaalamu mwandamizi wa madini, mwaka 2002-2004, mtaalamu wa miamba mkuu na mbobezi  wa madini, mwaka 2004-2006, alikuwa ofisa mawasiliano na mwaka 2006 mpaka 2011, alikuwa kamishna wa madini.
Ngeleja
Kwa upande wake Ngeleja aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kuanzia mwaka 2008 hadi 2012, alisema hataki kuzungumzia juu ya kilichoelezwa na kamati hiyo ikiwamo kutajwa kwake, bali anachoweza kusema ni kuwa, Rais Magufuli ameonesha uzalendo. 
“Sitaki kuzungumza yaliyo kwenye ripoti ya uchunguzi, ila tu nisema kwa wale tuliosikiliza wakati ripoti inawasilishwa na wakati Rais mwenyewe anazungumza, unaona hisia za uzalendo ambazo Rais anazo, na ameeleza kwa uchungu mkubwa namna ambavyo tunastahili kupata zaidi kuliko tunachopata sasa.
“Lakini jambo kubwa alilolifanya, amesema atamkabidhi taarifa (Spika wa Bunge), kwa sababu msingi wa mambo yote haya ni sera na sheria za nchi.
“Kwamba sisi kama Bunge tutimize wajibu wetu tuhakikishe mapungufun yote yaliyo pale tunayafanyia kazi, lakini kikubwa  amesema chenji (fedha zilizokwepwa na migoni) yetu irudi na amewakaribisha wawekezaji wakae mezani, lakini baada ya kuzingatia masilahi ya upande wetu, ni jambo jema.
 “…wakati nachangia bajeti ya Wizara ya Nishati nilisema, sheria hata tuliyo nayo sasa tungekuwa tumeitekeleza vizuri tusingekuwa hapa tulipo na moja ni kuhusu mikataba iliyofungwa kabla ya mwaka 2010,” alisema
Alisema kifungu cha 116 cha Sheria ya Madini, kinasema mikataba yote iliyofungwa kabla ya kutungwa kwa sheria ya madini ya mwaka 2010, inatakiwa iheshimu na  itambulike kwa utaratibu wa sheria hiyo.
“Kwenye kifungu cha 11 cha hii sheria ya madini, inasema kila baada ya miaka mitano baada ya kuanza kutumika hii sheria, mikataba yote ya madini ipitiwe upya.
“Mimi nilijiuzulu uwaziri Mei 4, 2012, sasa ni miaka mitano imepita, na wakati najiuzulu mimi tulikuwa tumemaliza kutunga kanuni, ninachotaka kusema ni kwamba kupitia hicho kifungu cha 11 hilo ndilo dirisha la kujadiliana yale ambayo kipindi kile kilishindikana,” alisema
Waziri huyo wa Nishati na Madini wa zamani, alisema kuwa kifungu cha 10 cha sheria hiyo kimeweka wazi namna Serikali inavyoweza kumiliki hisa kimkakati kwa kutumia dirisha hilo.
“Utaratibu huo ndiyo tumeutumia kwa Mchuchuma na Liganga, ambapo serikali ina asilimia 20 za bure, Ngaka ina asilimia 30 za bure, hayo ndiyo niliyosema,” alisema Ngeleja.


MWANDISHI:Fredy Azzah-Dodoma


Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

WASTANI WA ADA ZA VYUO VIKUU BORA ZAIDI DUNIANI.

            Elimu ya juu ya kupokea nje ya nchi (Nchi zilzo endelea) daima imekuwa kiwango cha kutambuliwa sana, na wanafunzi kutoka duniani kote siku zote wana ndoto kuhusu hilo.             Tovuti ya Bright Side imeamua kujua gharama za sasa za kujifunza * kwa wanafunzi wa kimataifa katika vyuo vikuu vya juu vya dunia, na tungependa kushiriki habari hii na wewe. * Wastani wa kila mwaka ada ya mafunzo ya shahada ya kwanza ; MAREKANI; Kwa maelezo zaidi kuhusiana na chuo hiki bonyeza hapa: http://www.harvard.edu/ Kwa maelezo zaidi kuhusiana na chuo hiki bonyeza hapa:  http://web.mit.edu/ UINGEREZA;     Kwa maelezo zaidi kuhusiana na chuo hiki bonyeza hapa; http://www.cam.ac.uk/     Kwa maelezo zaidi kuhusiana na chuo hiki bonyeza hapa: http://www.ox.ac.uk/ USWISI (SWITZERLAND ):     Kwa maelezo zaidi kuhusiana na chuo hiki bonyeza hapa:...

ORODHA YA NCHI ZA KWANZA NA ZA MWISHO KWA AMANI DUNIANI.

Marekani:  Ripoti ya Taasisi ya Uchumi na Amani imepata mataifa kumi tu ulimwenguni ambayo hayapo katika vita na migogoro kabisa. Kwa mujibu wa Ripoti ya Kimataifa ya Amani 2016, Botswana, Chile, Costa Rica, Japan, Mauritius, Panama, Qatar, Uswisi, Uruguay na Vietnam ndio nchi pekee ambazo hazipo kwenye vita wala migogoro yeyote ile ya kuhatarisha amani.. Iceland inaongoza orodha ya nchi zinazoongoza kwa amani ulimwenguni, ikifuatiwa na Denmark, Austria, New Zealand, Ureno, Jamhuri ya Czech, Uswisi, Canada, Japan na Slovenia - wakati Marekani ikiwa kwenye nafasi ya 103. Palestina imepanda kutoka nafasi ya 163 mpaka nafasi ya 148. Syria iliyoharibiwa na vita imewekwa chini ya orodha, chini kuliko Sudan Kusini, Iraq, Afghanistan, Somalia, Yemen, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ukraine, Sudan na Libya. "Ripoti inalinganisha amani duniani kwa kutumia mandhari tatu pana: hali ya utulivu na usalama katika jamii; kiwango cha mgogoro wa ndani au wa kimataifa; na kiwango cha kije...

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA GAMBIA AMTAKA RAIS WA TOGO KUACHIA MADARAKA KWA HIARI.

RAIS WA TOGO, FAURE GNASSINGBE. BANJUL, Oktoba 23 (Reuters) "Rais wa Togo Faure Gnassingbe anapaswa kujiuzulu mara moja na Umoja wa Afrika na kanda ya kikanda ya Afrika Magharibi ECOWAS inapaswa kumshawishi kushuka ikiwa hawaja fanya hivyo",  Waziri wa Mambo ya Nje wa Gambia Ousainou Darboe amesema. Maoni ya Darboe ni ishara ya mwanzo kwamba yuko dhidi ya Gnassingbe ambaye alinyakua madaraka kwa nguvu mwaka 2005 baada ya kifo cha baba yake ambaye alikuwa ametawala tangu mwaka 1967. Togo ni inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa ambao takribani watu 10 wameuawa katika maandamano tangu Agosti. "Nadhani Umoja wa Afrika na ECOWAS inapaswa kushiriki na kumshawishi rais wa Togo kung'ooka ," Darboe aliiambia Shirika la habari la Uingereza (Reuters) mwishoni mwa wiki hii, akiongezea kuwa nchi nyingine zinahitaji kushiriki. "Wakati serikali ya Togo inakiuka kanuni zinazokubalika sidhani kama suala hili linapaswa kuchukuliwa kama ni mambo ya ndani ya nd...

SABABU YA ZIPU NYINGI KUWA NA HERUFI "YKK".

Ikiwa umewahi kuchunguza kwa ukaribu zipu kwenye nguo zako nyingi, utakua tayari umeona herufi zinazosomeka "YKK," katika herufi kubwa, kwa mengi yao.Herufi hizi zipo kwenye kila kitu kutoka kwenye nguo za jeans, makoti hata kwenye mabegi. Herufi hizo zinasimama kwa niaba ya "Yoshida Kogyo Kabushikikaisha" ambayo, kutoka kwenye lugha ya Kijapani, inaelezea  "Yoshida Company Limited" yaani "Kampuni ya Yoshida"  Kampuni hii ni ya mtengenezaji wa zipu aitwaye Tadao Yoshida, ambaye aliianzisha mwaka wa 1934. Kwa wastani, kampuni hiyo inatengeneza nusu ya zipu duniani, ambayo ni zaidi ya zipu bilioni 7 kila mwaka. Kwa uhalisia Yoshida hakua mvumbuzi wa zipu duniani, zipu zilivumbuliwa na Mmarekani, Whitcomb L. Judson, miaka ya 1890.  Kampuni yake sasa ipo,  na inabuni na kutengeneza zipu za kisasa ikijulikana kama Talon, Inc. Bidhaa za kampuni hiyo hutumiwa makampuni kama Brooks Brothers na Uniqlo. Lakini YKK ina sifa isiyofananishik...

UGANDA IMEWAFUKUZA WATAALAM WA KIJESHI KUTOKA KOREA YA KASKAZINI.

Uganda imefukuza wataalamu wa kijeshi wa Korea Kaskazini na wawakilishi wa makampuni ya Kaskazini ya Korea, ikiwa ni pamoja na mfanyabiashara wake mkubwa wa silaha za juu kutokana na mataifa ya Kiafrika kukabiliwa na shinikizo la kuzingatia vikwazo vya Umoja wa Mataifa(UN) juu ya mpango wa silaha za nyuklia wa Pyongyang. "Raia wa Korea ya Kaskazini waliobaki katika taifa hilo la Afrika Mashariki ni wanadiplomasia na watu binafsi tu ", Okello Oryem, naibu waziri wa mambo ya kigeni, aliiambia The Associated Press. "Tunafuatana kabisa," alisema Oryem, akiongezea kwamba Uganda ina uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia na Korea Kaskazini. Uganda hasa ilidai kuondoka kwa watu wanaowakilisha Shirika la Biashara la Maendeleo ya Madini ya Korea. Ni mkataba wa msingi wa Korea Kaskazini na chini ya vikwazo vya U.N. na U.S. Uhamisho huo unaashiria mabadiliko ya sera kwa serikali ya Uganda, ambayo hapo awali ilikuwa na mahusiano ya mazuri na Pyongyang. Korea ya Kaska...

PAPA FRANCIS ASHINDANISHWA NA PABLO ESCOBAR KWA KUHESHIMIWA NCHINI COLOMBIA.

Medellín (Colombia) (AFP):  Katika saluni yake ya nywele, Yamile Zapata anatumia faida ya ziara ya Papa Francis ili kuuza pete za funguo zenye picha ya kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani. Lakini anadai sio ambapo pesa halisi iko kwenye mji wa Medellin nchini Colombia. Zawadi nyingi anazouza katika mji huu wa Colombia hubeba uso wa "mtakatifu" na shujaa wake mwenyewe: Pablo Escobar. Wakati Francis alikuwa akihudumia na kufundisha kama kuhani wa Yesuit katika miaka ya 1980, Escobar alikuwa akiua mamia ya watu na kufanya biashara ya madawa ya kulevya ya mabilioni ya dola za kimarekani. "Kila mtu anataka picha za papa sasa, lakini picha za Pablo zinauzika vizuri zaidi," , alisema Zapata, mwenye umri wa miaka 34, wakati ambao jiji hilo limeandaliwa kwa ajili ya mkutano wa Papa Francis wa wazi siku ya Jumamosi. PETE ZA FUNGUO ZENYE PICHA ZA PAPA FRANCIS NA PABLO ESCOBAR ZIKIWA ZINAUZWA KWENYE MITAA YA JIJI LA MEDELIN, COLOMBIA. Francis alitoa mane...

MCHEZAJI WA ZAMANI WA UINGEREZA AMESEMA ALICHEZA NA WACHEZAJI WATATU MASHOGA KWENYE TIMU.

Carl Hoefkens (jezi no.2) alichezea West Bromwich Albion na Stoke City wakati wa enzi zake ligi kuu ya England. Beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza amesema alicheza pamoja na wachezaji wenzake wawili wa mashoga ndani ya timu, na mmoja alikua na jina kubwa. Carl Hoefkens, West Bromwich Albion na Stoke City siku za nyuma, anasema wachezaji hao walikua wazi na hawakujificha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingawa bado hawajulikani kwasababu ya maombi yao wenyewe ya kuomba kutotangazwa. Justin Fashanu, ambaye alijiua mwaka 1998, alikuwa mchezaji wa mwisho wa kazi nchini England kuja nje kama mashoga - mwaka 1990. Hoefkens alipokua (kushoto), alipokua anachezea Stock  City. Hoefkens aliyecheza Uingereza kwa miaka minne, akiondoka mwaka 2009, alidai kuwa mchezaji mwenzake mmoja wa timu alikua anaweza kuja kwenye uwanja wa mafunzo ya klabu na mpenzi wake wa kiume  lakini aliwaomba wenzake kutokuwaambia watu wangine wa nje ya timu. 'Nilicheza pamoja n...