Kutoka Gazeti TAIFA LEO | Nairobi, Kenya:
Katika juhudi zake za kukomesha mzozo wa kisiasa ambao umekumba Kenya tangu uchaguzi mkuu wa Agosti 8, 2017, imefichuliwa kwamba nchi hiyo yenye ushawishi mkubwa ulimwenguni inapendekeza Bw Odinga apandishwe hadhi kuwa kiongozi wa taifa na apewe mamlaka makubwa katika taifa.
Katika pendekezo hilo, Bw Odinga atapewa ofisi, wafanyakazi, msafara wa magari sawa na wa kiongozi wa nchi na marupurupu ambayo yatamwezesha kuzuru kote ulimwenguni kuwakilisha Kenya na kuhutubu kuhusu demokrasia.
Kiongozi huyo wa Chama cha ODM pia atalipwa marupurupu ya kustaafu kwa msingi wa miaka mingi ambayo ametumikia umma na ameahidiwa juhudi zake za kupigania mageuzi hasa haki katika uchaguzi zitaungwa mkono.
Duru zilisema mapendekezo hayo yaliwasilishwa kwa Bw Odinga na Balozi wa Marekani nchini Kenya, Robert Godec, ambaye amekuwa akikutana na wanasiasa wa NASA na Jubilee.
Haikuwezekana kuthibitisha haya kutoka kwa ubalozi wa Marekani nchini kufikia wakati wa gazeti hili kuchapishwa.
Hata hivyo, inasemekana Bw Odinga alikataa mapendekezo hayo kwa vile hayatatui maslahi ya Wakenya ambao wanataka kuona haki katika uchaguzi baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuvuruga uchaguzi wa urais wa Agosti 8, 2017.
“Hawajaeleza kwa kina kuhusu itakavyokuwa bali wanazungumza tu kuhusu kujumuisha wadau zaidi. Lakini nimewahi kusema wanaingilia masuala ya Kenya.
Hawana haki kuja kutuambia nani anafaa kuwa hiki wala kile. Tunazungumza kuhusu wizi wa kura na nia yetu ni kuleta mabadiliko yatakayotenda haki uchaguzini,”
Bw Odinga akasema kwa simu Jumapili.
Mwanasiasa mmoja wa NASA aliambia ‘Taifa Leo’ kwamba Bw Odinga pia alisema mapendekezo hayo hayazingatii maslahi ya vinara wengine wa muungano huo.
Kinara huyo alinukuliwa kumwambia Bw Godec:
“Tuseme nimekubali, nitawafanyia nini vinara wenzangu katika NASA?”
Kiranja wa Wachache katika Bunge, Bw Junet Mohammed, alisema hana habari kuhusu mapendekezo hayo na kusisitiza kuwa kulingana na NASA Bw Odinga anafaa kuwa rais.
“Uongozi wa taadhima haupeanwi kwa mtu. Bw Odinga ameupata kupitia mchango wake na vitendo vyake kwa nchi hii na mataifa mengine ya Afrika na hakuna anayeweza kumkabidhi wadhifa huo,”
akasema Bw Junet.
Lakini mwanasiasa mwingine wa NASA alisisitiza kuwa Bw Odinga amekabidhiwa mapendekezo hayo ingawa changamoto iliyopo ni kwamba inashukiwa yalibuniwa na Jubilee ambayo imekuwa ikimshinikiza astaafu katika siasa.
“Tuna kila sababu ya kuamini kwamba haya ni mapendekezo ya kibinafsi ya Godec au mbinu ya Jubilee ambayo balozi huyo amekubali kuhusika,” akasema mwanasiasa huyo ambaye aliomba asitajwe jina kwani hana idhini rasmi kuzungumzia suala hilo.
CHANZO:
public class HelloWorld { public static void main(String[] args) { System.out.println("Hello World"); } } <script type="text/javascript"> ( function() { if (window.CHITIKA === undefined) { window.CHITIKA = { 'units' : [] }; }; var unit = {"calltype":"async[2]","publisher":"Kioo17swahili","width":550,"height":250,"sid":"Chitika Default"}; var placement_id = window.CHITIKA.units.length; window.CHITIKA.units.push(unit); document.write('<div id="chitikaAdBlock-' + placement_id + '"></div>'); }()); </script> <script type="text/javascript" src="//cdn.chitika.net/getads.js" async></script>
Comments
Post a Comment