Henrikh Mkhitaryan atatupwa kando na meneja wa Manchester United Jose Mourinho ili apate nafasi ya kumsajili jiungo wa Arsenal, Mesut Ozil, kulingana na taarifa.
Bosi huyo wa Manchester United anajua lazima apunguze kikosi chake kama atataka kumsajili Ozil kutokana na madai ya mshahara mkubwa ya bingwa huyo wa Kombe la Dunia.
Kiungo huyo mchezeshaji huyo ambaye mkataba wake Arsenal umalizika mwishoni mwa msimu huu, amekuwa akiomba mshahala wa Pauni Laki Tatu (£ 300,000) kwa wiki ili kukubali mkataba mpya wa kuendelea kuchezea Arsenal.
Gazeti la 'The Mirror' la Uingereza limeripoti kwamba Mourinho ameamua Mkhitaryan, ambaye alijiunga na klabu kutoka Borussia Dortmund mwaka 2016, anaweza kuwa mchezaji kuondoka
Ni uchaguzi wa mantiki kulingana na hali ya sasa ya mchezaji huyo katika kikosi cha Manchester United. Mchezaji huyo kutoka Armenia ameachwa mechi nane za mwisho na Mourinho huku akisema kuwa haamini kama kiungo huyo anastahilo kukukaa katika benchi la timu yake.
'Ninaweza tu kuwa na wachezaji sita kwenye benchi na ninajaribu kuwa na usawa kwenye benchi,'
alisema kocha huyo wa Kireno baada ya kumwacha Mkhitaryan nje na kushinda 1-0 dhidi ya Bournemouth.
"Nilikuwa na mabeki wawili ambao wanaweza kucheza katika nafasi mbalimbali, nina Ashley Young ambaye anaweza kucheza kama winga na beki wa pembeni, [Ander] Herrera ni mchezaji wa katikati, Zlatan [Ibrahimovic] ni mshambuliaji, [Marcus] Rashford ni mshambuliaji wa pili na winga.
'Kuwa na Mkhitaryan ina maana nimkose mmoja wao na naamini wengine wanastahiki.'
Mara ya mwisho kwa Mkhitaryan kuanza mechi ilikua ni mechi waliyopoteza kwa 1-0 dhidi ya Chelsea mwanzoni mwa Novemba na kuonekana kwake peke yake tangu wakati huo kutoka benchi dhidi ya Brighton mwishoni mwa Novemba.
CHANZO:
Comments
Post a Comment