Maafisa wa polisi na wahudumu wa uwanja walilazimika kuwatenganisha wachezaji wasiopungua 20 na wafanyakazi wa timu za Manchester United na Manchester City baada ya kupigana katika vurugu kubwa ilijitokeza kwenye njia za kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye uwanja wa Old Trafford jana(jumapili, 20, Desemba, 2017).
Kwa mujibu wa gazeti la Guardian la Uingereza chupa na ngumi zilirushwa baada ya mchezo huo ambao Manchester City ilishinda 2-1 dhidi ya mahasimu wao wa jiji, Manchester United na msaidizi wa kocha meneja wa Manchester city, Pep Guardioa, Mikel Arteta aliondoka akiwa ametapakaa damu chini ya uso wake.
Machafuko hayo yalidaiwa kuanza baada ya meneja wa Manchester United, Jose Mourinho kugonga mlango wa chumba cha wapinzani wake kuwaambia wachezaji hao kupunguza sauti ya muziki wao.
Punde baadae Mourinho alijikuta katika mzozo mwingine na kipa wa Manchester city, Mbrazili Ederson, ambapo Mourinho alidai mchezaji huyo alikua anapoteza muda kwa makusudi uwanjani, kabla ya kupiga kelele kwa Kiingereza:
"Wewe ... onesha heshima...kwani wewe ni nani?"
Romelu Lukaku amedaiwa kuwa amehusika sana katika vurugu iliyofuata baada ya mechi ambayo mtu mmoja ameelezea kama kulifanana na mapigano ya kwenye vilabu vya pombe, na inaaminika kwamba tukio hilo lilikuwa kubwa zaidi kuliko "mapigano ya Buffet" vya mwaka 2004, wakati Cesc Fabregas wa Arsenal alimporushia chakula aina ya pizza meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson.
Wachezaji wa Manchester United waliripotiwa walihisi kuwa kelele kutoka chumba cha mavazi ya Manchester City zilikuwa kubwa kwa sauti, na kwamba waliacha mlango wazi kwa makusudi.
Kulikuwa na ripoti kwamba Mourinho alipigwa na chupa ya plastiki na maziwa, kabla ya kulalamika kwa mwamuzi wa mechi hiyo Michael Oliver kuhusu tukio hilo wakati wa mechi.
CHANZO:
esquire.co.uk
Comments
Post a Comment