Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza .
Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza za kusafiria kama ilivyokuwa nchi za afrika Mashariki.
Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni nchi ngapi ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza (viza on arrival).
"Zipo nchi 16 kwa Afrika ambazo watanzania wanaweza kuzitembelea bila ya kuwa na viza na duniani zipo 67" alisema Masauni.
Aidha Massauni amezitaja nchi hizo kuwa ni Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, GuineaBissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo.
Pamoja na hayo Masauni amesema zipo nyingine ndani ya umoja wa Jumuiya ya Madola lakini haziwezi kuwapatia fursa watanzania kutumia 'viza on arrival'.
"Ni kweli nchi za Jumuiya Madola zinautaratibu wa kutembeleana wananchi wake bila ya kuwa na Viza lakini kama nilivyo jibu katika swali langu la msingi kwamba ushirikiano na matengemano hayo ya jumuiya ya madola utaratibu wake unaweza kubadilika kulingana na mahusiano na hali ya kiusalama kwa hiyo siyo jambo la kushangaza kuona India na Nigeria kwamba nchi hizi mbili zipo kwenye uanachama wa Jumuiya ya Madola lakini utaratibu wa viza kuna 'level' unakuwa hautumiki" alisisitiza Masauni.
KUTOKA JAMII FORUMS
kunautaratibu wa kila nchi katika kuruhusu wageni kuingia nchini mwao. Nchi zote duniani huitaji visa itakayokupa ruhusa wewe kukaa nchini mwao kwa kipindi utakachokuwa umepewa.
Lakini kutokana na urafiki na makubaliano ambayo huwa yanafanywa na baadhi ya nchi juu ya uhuru wa kutembeleana kwa watu wao, huwa wanaamua kutoa kikwazo cha visa na hivyo kururhusu watu wao kutembeleana pasipokuwa na visa.
Tanzania inajumla ya nchi 76 ambazo mtanzania anaweza kutembelea pasipokuwa na visa ya kumuwezesha kuingia ndani ya nchi hizo.
Baadhi ya nchi hizo ni Albania, Cook Islands, Djbouti, Dominica, Ethiopia, Ecuador, Fiji, Grenada, Gambia, Georgia, Haiti, Nepal, Namibia, St Lucia, Singapore, Seychelles, Swaziland, Tuvalu, Togo, Trinidad & Tobago, Timor-Leste, Uganda, Vanuatu, Zambia, Zimbabwe
zingine hizi hapaAntigua & Barbuda
Albania *
Armenia
Azerbaijan
British Virgin Islands
Barbados
Bangaladesh
Botswana
Burundi
Bahamas
Belize
Bermuda
Bolivia
Cambodia
Cayman Islands
Cape Verde
Comoros
Cook Islands
Djibouti
Dominica
Ethiopia
Ecuador
Egypt **
Fiji
Grenada
Gambia
Guinea
Georgia
Haiti
Hong Kong (3months Visa upon arrival)
Jamaica
Jordan *
Kenya
Kosovo
Laos
Lebanon *
Lesotho
Libya *
Liberia
MacauMalaysia (1 month visa upon arrival)
Madagascar
Maldives
Malawi
Mauritius
Micronesia
Mozambique
Montserrat
Mongolia
Nauru
Niue
Nepal
Namibia (1 month visa upon arrival)
Nicaragua
Palau
Philipines
Qatar *
Rwanda
Samoa
Suriname *
St.Kitts & Nevis
St.Vincent & Grenadines
St. Lucia
Sierra Leone
Singapore (1 month visa upon arrival)
Seychelles
Swaziland
Tuvalu
Togo
Turkmenistan *
Trinidad & Tobago
Timor-Leste
Uganda
Vanuatu
Zambia
Zimbabwe
In the case of Egypt, travelling without visa
Comments
Post a Comment