Ulimwengu wa filamu za Hollywood na muziki wa Hip Hop juzi ulipatwa na mshangao baada ya mtayarishaji wa filamu inayohusu maisha ya hayati Tupac Shakur ,L.T Hutton kuelezea sababu zilizomfanya kumbadilisha muongozaji wa filamu hiyo kutoka John Singleton na kumuweka muongozaji Benny "Boom" Douglas.
Filamu hiyo inayoitwa "all eyez on me" tayari imekwisha andaliwa na inatarajiwa kuzinduliwa leo tarehe 16 Juni 2017.
Akizungumza kwenye mahojiano redioni L.T Hutton amewashtusha watu wengi baada ya kudai kwamba walishindwana na muongozaji wa mwanzo bwana John Singleton sababu muongozaji huyo aling'ang'ania kuwepo kwa matukio (scene) ambazo kwa maoni yake zisingependeza.
Matukio ambayo John Singleton alipenda yawepo katika filamu hiyo ni pamoja na kutaka filamu hiyo ianze na scene ya Tupac akilazimisha kumlawiti msichana wa kizungu.!!!
Singleton pia alitaka kuwepo na scene ya Tupac akibakwa gerezani.!!!
Kana kwamba haitoshi muongozaji huyo alitaka kuwepo na scene inayoonesha mama yake Tupac, Hayati Afeni Shakur akifanya mapenzi na watu wawili (Threesome) chumbani.
Tazama Trailer ya filamu hiyo hapa chini:
Tazama video ya mahojiano hayo hapa chini:
https://youtu.be/TgBGX5OT-ao
VYANZO : http://icecreamconvos.com/wtf-john-singleton-wanted-anal-sex-afeni-threesome-tupac-jail-rape-scene-eyez-video/
Comments
Post a Comment