LUCA MODRIC. |
Mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham alikuwa shahidi muhimu katika kesi ya zamani ya mkurugenzi mkuu wa zamani wa timu ya Dinamo Zagreb, Zdravko Mamic jijini Osijek.
Modric alitoa ushahidi wiki mbili ziliyopita katika kesi ya rushwa wiki inayomkabili Mamic kwa kukwepa kodi ya paundi milioni moja nukta nne (£ 1.4m) na ubadhilifu wa paundi milioni kumi nukta tano (£ 10.5m), ya pesa ya klabu pamoja na nduguye Zoran, mkurugenzi wa klabu Damir Vrbanovic na mfanyakazi wa utawala wa kodi Milan Pernar.
MODRIC AKIINGIA MAHAKAMANI. |
Kipande kingine cha kesi hiyo kilikuwa ni Mamic kinyume cha sheria kuchukua paundi milioni kumi na sita nukta tano ( £ 16.5m) ikiwa ni sehemu ya pesa waliyolipwa Dynamo kwa kumuuza Modric kwa Tottenham Hotspurs mwaka 2008.Hivyo Modric aliitwa kutoa ushahidi wa nini kilitokea.
MODRIC AKIWA ANACHEZEA DYNAMO ZAGREB. |
Modric mwanzoni alikubali kwamba kweli ilikua ni kesi kabla ya kukataa na kusema walikua wamemchanganya.
"Wakati wa kusema juu ya hilo, nilikuwa nikisema juu ya mkataba wa kibinafsi kati ya Mamic na mimi, ambayo ilidhibiti mgawanyiko wa ada ya uhamisho," alisema.
MODRIC AKIWA MAHAKAMANI. |
Lakini sasa Ofisi ya Mwanasheria wa Jimbo la Croatia imeanza uchunguzi juu ya ushahidi wa Modric, wakiwa na wasiwasi kwamba aliwaambia uongo.
Ikiwa itathibitika kupatikana na hatia ya kudanganya, Modric anaweza kukabiliana na kifungo gerezani kati ya miezi sita na miaka mitano jela.
VYANZO:http://www.mirror.co.uk/sport/football/news/luka-modric-could-face-jail-10651016?ICID=FB_mirror_main
Comments
Post a Comment