Skip to main content

WALICHOJIBU CHENGE ,NGELEJA NA DK.KAFUMU BAADA YA RIPOTI YA PILI YA RAISI.



              VIGOGO waliotajwa katika ripoti ya pili ya kuchunguza makontena yenye mchanga wa madini (makinikia)  kuisababishia Serikali hasara ya matrilioni ya fedha kupitia sekta ya madini, walipokuwa wakihudumu katika nyadhifa zao serikalini wamevunja ukimya.
Vigogo hao wamezungumzia ripoti hiyo ya pili iliyowasilishwa kwa Rais Dk. John Magufuli Ikulu Dar es Salaam jana, ambapo kamati husika ilichunguza hasara ambayo nchi imepata tangu 1998 usafirishaji wa mchanga wa dhahabu nje ya nchi ulipoanza.

Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM), alipoulizwa maoni yake juu ya kutajwa na kamati hiyo, alisema hataki kuzungumza chochote juu ya ripoti hiyo, huku Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), akisema sheria ya madini ya 2010 ingefuatwa, nchi isingekuwa hapa ilipo.
Kwa upande wake Kamishna wa Madini wa zamani, Dk. Dalaly Kafumu, alisema kwa sasa  hawezi kuzungumza jambo lolote kwa kuwa ni yeye ni mmoja wa watuhumiwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo.
Chenge
Baada ya kutoka kwenye kipindi cha asubuhi cha Bunge ambacho alikuwa akikiendesha, Chenge alipotakiwa kuzungumzia ripoti hiyo, alijibu kwa ufupi.
“Sizungumzi na mtu,” na alipoulizwa kama hata salamu hataki, alisema. “Sizungumzi na mtu mimi,” alisema Change ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Chenge alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kati ya 1972 na 1990, ambapo mwaka 1993 aliteuliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali nafasi ambayo alidumu nayo hadi mwaka 2005.
Dk. Kafumu
MTANZANIA ilimpomtafua Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM), ambaye ametajwa kutaka kuingilia ripoti ya kamati ya kwanza iliyochunguza mchanga huo, alisema hataki kuzungumza chochote kwa sasa ingawa anaamini kila kitu kiko sawa.
“Kwa kuwa nimetajwa kama mtuhumiwa, sitaki kusema kitu kwa sasa kwa sababu hili ni sawa na jambo lililo mahakamani tu kwa kuwa wamesema tutahojiwa, lakini kila kitu kiko sawa,” alisema Dk. Kafumu.
Alipoulizwa kama ni kweli alikutana na Profesa Abdulkarim Mruma, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya kwanza na ni nini walichozungumza, Dk. Kafumu alisema. “Nimeshasema no comment (sina la kusema ),” alisema Dk. Kafumu.
Dk. Kafumu ni moja ya watumishi waliohudumu ndani ya Wizara ya Nishati na Madini ambapo alifanyakazi kazi ndani ya wizara hiyo kuanzia mwaka 1983 hadi 2011, alipoacha na kwenda kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa marudio wa Igunga, baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Rostam Aziz.
Taarifa zilizopo kwenye tovuti ya Bunge zinaonesha, mwaka 1983 mpaka 1987, Dk. Kafumu alikuwa mtaalamu wa miamba na madini wa wizara hiyo, mwaka 1987 mpaka 1992, mkufunzi na mtafiti wa madini, mwaka 1992 mpaka 2002 akawa mtaalamu mwandamizi wa madini, mwaka 2002-2004, mtaalamu wa miamba mkuu na mbobezi  wa madini, mwaka 2004-2006, alikuwa ofisa mawasiliano na mwaka 2006 mpaka 2011, alikuwa kamishna wa madini.
Ngeleja
Kwa upande wake Ngeleja aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kuanzia mwaka 2008 hadi 2012, alisema hataki kuzungumzia juu ya kilichoelezwa na kamati hiyo ikiwamo kutajwa kwake, bali anachoweza kusema ni kuwa, Rais Magufuli ameonesha uzalendo. 
“Sitaki kuzungumza yaliyo kwenye ripoti ya uchunguzi, ila tu nisema kwa wale tuliosikiliza wakati ripoti inawasilishwa na wakati Rais mwenyewe anazungumza, unaona hisia za uzalendo ambazo Rais anazo, na ameeleza kwa uchungu mkubwa namna ambavyo tunastahili kupata zaidi kuliko tunachopata sasa.
“Lakini jambo kubwa alilolifanya, amesema atamkabidhi taarifa (Spika wa Bunge), kwa sababu msingi wa mambo yote haya ni sera na sheria za nchi.
“Kwamba sisi kama Bunge tutimize wajibu wetu tuhakikishe mapungufun yote yaliyo pale tunayafanyia kazi, lakini kikubwa  amesema chenji (fedha zilizokwepwa na migoni) yetu irudi na amewakaribisha wawekezaji wakae mezani, lakini baada ya kuzingatia masilahi ya upande wetu, ni jambo jema.
 “…wakati nachangia bajeti ya Wizara ya Nishati nilisema, sheria hata tuliyo nayo sasa tungekuwa tumeitekeleza vizuri tusingekuwa hapa tulipo na moja ni kuhusu mikataba iliyofungwa kabla ya mwaka 2010,” alisema
Alisema kifungu cha 116 cha Sheria ya Madini, kinasema mikataba yote iliyofungwa kabla ya kutungwa kwa sheria ya madini ya mwaka 2010, inatakiwa iheshimu na  itambulike kwa utaratibu wa sheria hiyo.
“Kwenye kifungu cha 11 cha hii sheria ya madini, inasema kila baada ya miaka mitano baada ya kuanza kutumika hii sheria, mikataba yote ya madini ipitiwe upya.
“Mimi nilijiuzulu uwaziri Mei 4, 2012, sasa ni miaka mitano imepita, na wakati najiuzulu mimi tulikuwa tumemaliza kutunga kanuni, ninachotaka kusema ni kwamba kupitia hicho kifungu cha 11 hilo ndilo dirisha la kujadiliana yale ambayo kipindi kile kilishindikana,” alisema
Waziri huyo wa Nishati na Madini wa zamani, alisema kuwa kifungu cha 10 cha sheria hiyo kimeweka wazi namna Serikali inavyoweza kumiliki hisa kimkakati kwa kutumia dirisha hilo.
“Utaratibu huo ndiyo tumeutumia kwa Mchuchuma na Liganga, ambapo serikali ina asilimia 20 za bure, Ngaka ina asilimia 30 za bure, hayo ndiyo niliyosema,” alisema Ngeleja.


MWANDISHI:Fredy Azzah-Dodoma


Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

MCHEZAJI WA ZAMANI WA UINGEREZA AMESEMA ALICHEZA NA WACHEZAJI WATATU MASHOGA KWENYE TIMU.

Carl Hoefkens (jezi no.2) alichezea West Bromwich Albion na Stoke City wakati wa enzi zake ligi kuu ya England. Beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza amesema alicheza pamoja na wachezaji wenzake wawili wa mashoga ndani ya timu, na mmoja alikua na jina kubwa. Carl Hoefkens, West Bromwich Albion na Stoke City siku za nyuma, anasema wachezaji hao walikua wazi na hawakujificha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingawa bado hawajulikani kwasababu ya maombi yao wenyewe ya kuomba kutotangazwa. Justin Fashanu, ambaye alijiua mwaka 1998, alikuwa mchezaji wa mwisho wa kazi nchini England kuja nje kama mashoga - mwaka 1990. Hoefkens alipokua (kushoto), alipokua anachezea Stock  City. Hoefkens aliyecheza Uingereza kwa miaka minne, akiondoka mwaka 2009, alidai kuwa mchezaji mwenzake mmoja wa timu alikua anaweza kuja kwenye uwanja wa mafunzo ya klabu na mpenzi wake wa kiume  lakini aliwaomba wenzake kutokuwaambia watu wangine wa nje ya timu. 'Nilicheza pamoja n...

ORODHA YA NCHI 80 AMBAZO MTANZANIA ANARUHUSIWA KUINGIA BILA VIZA.

         Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza . Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza za kusafiria kama ilivyokuwa nchi za afrika Mashariki. Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni nchi ngapi ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza (viza on arrival). "Zipo nchi 16 kwa Afrika ambazo watanzania wanaweza kuzitembelea bila ya kuwa na viza na duniani zipo 67" alisema Masauni. Aidha Massauni amezitaja nchi hizo kuwa ni Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea­Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo. Pamoja na hayo Masauni amesema...

KIONGOZI MKUU WA UPINZANI NCHINI ZIMBABWE, MORGAN TSVANGIRAI AMEFARIKI DUNIA.

Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika Kusini, afisa mkuu wa chama chake cha MDC amesema. Bw Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 65, aliyekuwa waziri mkuu, alilipotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na saratani ya koloni. "Amefariki jioni hii, familia yake imenitaarifu"  Makamu wa Rais wa MDC, Elias Mudzuri aliliambia shirika la habari la Uingereza, Reuters. Morgan Tsvangirai alizaliwa mnamo Machi 10, 1952 huko Gutu, Zimbabwe. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa mgodi, fundi, na mkulima. Alihudhuria Shule ya Msingi ya Guco ya St. Marks. Kisha alihamishiwa Shule ya Msingi ya Chikara Gutu. Kwa elimu yake ya sekondari, alihudhuria Shule ya High Gokomere. Alikuwa waziri mkuu katika serikali ya mseto ya Zimbabwe tangu 2009 hadi 2013. Katika kazi yake ya awali alionekana kuwa mfanyakazi mwenye bidii sana na alifanya kazi katika mgodi wa madini ya nickel( kwa zaidi ya muongo mmoja. Alipanda cheo haraka kutambuliwa na akain...

MADAI YA CUBA KWAMBA WAZIRI MKUU WA CANADA NI MTOTO WA FIDEL CASTRO.

Pichani ni waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau (kushoto), na Rais wa zamani wa Cuba, Hayati Fidel Castro (kulia). Maelezo yaliyoandikwa na mtoto wa kwanza wa rais wa zamani wa Cuba , Fidel Castro, kabla ya kujiua yamelishtua taifa la Cuba wiki hii. Maelezo hayo yaliyoandikwa na mtoto huyo mkubwa wa mwanamapinduzi na rais wa zamani wa nchi hiyo yalikuwa ya kushangaza baada ya  kuwa na madai ya kuwa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ni mtoto wa nje wa baba yake marehemu Fidel Castro. Maelezo hayo yaliyoandikwa kwa mkono na mtoto huyo wa Fidel Castro aliyejiua siku chache zilizopita kwa msongo wa mawazo, Fidel Castro Diaz-Balart, aliyekuwa na umri wa miaka 68, yalionekana kuthibitisha uvumi wa muda mrefu nchini Cuba kwamba Fidel Castro ni baba wa damu wa waziri mkuu wa sasa wa Canada, Justin Trudeau ikiwa ni matokeo ya uhusiano wa siri wa kimapenzi na mke wa mwanasiasa maarufu wa Canada, Pierre Trudeau, Margaret Trudeau mwaka 1970. Kifo cha mwanasayansi wa ...

KASHFA YA MAPENZI KATI MH.MBOWE NA WEMA SEPETU.

MH.FREEMAN MBOWE AKIWA NA WEMA SEPETU. Siku chache baada ya ile skendo ya ngono iliyosababisha wakili na mshauri wa Chama cha ACT -Wazalendo , Bwana Albert Msando kujiuzulu kwenye nyadhifa yake ya chama ,yameibuka mangine kwenye chama kikuu cha upinzani Tanzania ,CHADEMA ,baada ya kusambaa kwa kipande cha sauti kinachodaiwa kua ni mazungumzo kati ya mwenyekiti wa chama hicho na mbunge wa Hai Mh.Freeman Mbowe na Miss Tanzania 2006 ,mrembo Wema Isack Sepetu. SIKILIZA HIVI VIPANDE VYA SAUTI: Bonyeza hapa chini kusikiliza maongezi hayo yanayodaiwa kuwa ni kati ya Wema Sepetu na Mh.Freeman Mbowe; Bonyeza hapa chini kusikiliza majibu ya Wema Sepetu; Bonyeza hapa chini kusikiliza majibu ya Mh.Freeman Mbowe; VYANZO: Jamii Forums,                   YouTube.com,                   Perfect255.com.                   

RAPA SNOOP DOGG AMETHIBITISHA MIPANGO YA KUHAMIA UGANDA.

Msanii wa muziki wa Hip Hop wa Marekani, Calvin Cordozar Broadus.Jr. maarufu kama Snoop Dogg amethibitisha kuwa anataka kuhamia Uganda baada ya rais wa Marekani, Donald Trump kudaiwa kuziita nchi za Afrika 'Shimo la Choo' . Snoop Doggy Dogg pia ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki, mtangazaji katika televisheni, na mwigizaji wa filamu ambaye alianza kupata umaarufu mkubwa katika muziki mwaka 1992 wakati alipogunduliwa na mtayarishaji Dr.Dre, na kushiriki katika nyimbo za Dr.Dre kama "Deep Cover", na kisha kwenye albamu ya kwanza ya Dr.Dre, ' The Chronic' . Kwa sasa tayari ameshauza albamu zaidi ya milioni 23 nchini Marekani na albamu milioni 35 duniani kote. Mmarekani huyo mweusi mwenye miaka 46 wa ambaye anajulikana kwa nyimbo zake za maarufu kama; The next episode, Drop it like it’s hot, beautiful, Lay low,  nk Juzi alirekodi kipande cha video na kukisambaza akisema kuwa anataka kuhamia chini Uganda. Tazama V...