WACHEZAJI LUIS SUAREZ,NEYMAR JR NA LIONEL MESSI WA FC BARCELONA WAKIWA WAMEVAA JEZI YA TIMU HIYO. |
Serikari ya Saudi Arabia imetangaza onyo na adhabu kali zitakazotolewa kwa mtu yeyote nchini humo atakaebainika kutumia bidhaa zinazohusiana na nchi jirani ya Qatar.
Hatua hiyo ya Saudi Arabia ni mwendelezo wa nchi hiyo ,Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE),Misri,Bahrain,Yemen,Maldives,Libya,Somaliland,Mauritania na Comoro kuiwekea vikwazo na kuitenga nchi ya Qatar kwa kuituhumu kujihusisha na vikundi vya kigaidi.
Serikali hizo za nchi nane zinaituhumu serikari ya Qatar kwa kuhatarisha usalama wa nchi zao hasa kwa kusaidia vikundi kama "Dola ya Kiisilamu" (ISIS) , Muslim Brotherhood na Serikali ya Iran.
Tayari serikari ya Falme za Kiarabu ilishatoa masaa 48 kwa raia wote wa Qatar kutojishughulisha na kitu chochote na kuondoka nchini kwao.
Kwa maana hiyo, maamuzi hayo yataathiri sio tu shughuli za kidiplomasia za Qatar ,bali na biashara ambazo serikali yake inamiliki au kua na hisa.
Moja kati ya makampuni ambayo yataathirika sana na hali hii ni Qatar Airways ambalo ni moja kati ya mashirika makubwa ya ndege duniani.Hii ni kutokana na ukweli kwamba Dubai na Abu Dhabi ni moja kati ya masoko makubwa ya shirika hilo.
MOJA KATI YA NDEGE ZA QATAR AIRWAYS IKIWA ANGANI. |
Kwa mfano, Saudi Arabia imetangaza kupiga marufuku mtu yeyote nchini humo kuvaa jezi za moja kati ya timu kubwa duniani Fc Barcelona ya Hispania.Hii ni kutokana na jezi hizo kuwa na jina la wadhamini likisomeka "Qatar Airways".
MOJA KATI YA JEZI ZA SASA ZA FC BARCELONA. |
Serikari hiyo imeonya kwamba adhabu ya atakae kaidi ni kufungwa miaka 15 jela au kulipa faini ya pauni za Uingereza laki moja na elfu ishirini (£120,000) , karibu Shilingi milioni 360 za kitanzania.
Hata hivyo athari sio kubwa sana kwa Fc Barcelona baada ya kuingia mkataba mpya wa miaka minne na kampuni ya kuuza bidhaa kwenye mitandao kutoka nchini Japan inayojulikana kama Rakuten.
NEMBO YA KAMPUNI YA RAKUTEN INAYOTARAJIWA KUTUMIWA NA FC BARCELONA MSIMU UJAO WA LIGI. |
VYANZO:
dailymail.com
http://uk.busiessinsider.com/qatar-airways-saudi-arabia-uae-ban-2017-6?r=US&IR=T
Comments
Post a Comment