EL HADJI DIOF (kombe la dunia 2002) |
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal El Hadji Diof ametangaza nia yake ya kutaka kugombea ubunge nchini humo.
Diof ambaye alistaafu kucheza soka mwaka 2015, alisema:
"Baadae yangu inajulikana, ndani ya miaka miwili nitaingia kwenye siasa sababu najua kuanzia kwenye hatua hiyo nitaweza kubadilisha mengi kwenye soka..."
"Ninapenda siasa, nina washauri wazuri Senegal na hayo ndio maisha yangu ya baadae sababu watu wa Senegal wanaweza kunisikiliza."
"Nimesoma kozi za juu kabisa za ukocha lakini nina mipango mizuri zaidi kwenye vitu ninavyotaka kufanya"
"Lakini nipo tayari kuishauri timu yangu (Senegal) muda wowote nikihitajika."
El Hadji Diof alikua mchezaji tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya Senegal iliyofuzu kucheza kombe la dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2002 na kua timu ya pili ya Afrika kufika hatua ya robo fainali baada ya Cameroon mwaka 1990.
Tazama kipande hiki cha video ya mechi kati ya Senegal na Ufaransa ,kombe la dunia 2002:
Diof pia amewahi kua mchezaji bora wa Afrika mara mbili.
EL HADJI DIOF AKIPOKEA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA. |
Mwaka 2002 baada ya kung'ara katika michuano ya kombe la dunia, alisajiliwa na timu ya Liverpool ya Uingereza kutoka Lens ya Ufaransa kwa Pauni Milioni 10 (£10 million). Baadaye alienda Bolton ,Sunderland, Blackburn, Rangers , Doncaster na Leeds kabla ya kumalizia soka katika klabu ya Sabah ya Malaysia.
Hata hivyo mwandishi wa jarida la Sun Football la Uingereza ,Steve Goodman ameandika kwenye makala yake kichwa cha habari "
"EL Hadji Diouf has threatened to wreak havoc in his home country … by going into POLITICS."
Akimaanisha:
" EL Hadji Diof ametishia kuleta madhara nchini kwake...kwa kuingia katika SIASA."
Hii nikutokana na na rekodi ya Diof ya kua na visa vingi ndani na nje ya uwanja wakati akicheza soka nchini Uingereza.
Kwa mfano, Diof aliwahi kusababisha utata mkubwa akiwa Liverpool baada ya kumtemea mate mshabiki wakati wa mechi ya Uefa Cup dhidi ya Celtics.
DIOF AKITOLEWA NJE BAADA YA KUMTEMEA MATE SHABIKI. |
Pia Diof aliwahi kusema kwenye mahojiano ya runinga kwamba nahodha wake wa zamani Steven Gerrard na mkongwe Jamie Gallagher hawana lolote kabisa kisoka.
VYANZO: https://www.thesun.co.uk/sport/football/2768873/el-hadji-diouf-politics-liverpool-bolton-leeds-rangers/?CMP=Spklr-_-Editorial-_-TheSunFootball-_-Football-_-FBLink-_-Statement-_-FBPAGE
Comments
Post a Comment