Skip to main content

ACACIA WAPINGA RIPOTI YA KAMATI YA PILI YA RAISI.






Mwitikio wa Acacia kwenye matokeo ya kamati ya pili ya Raisi.

Acacia imeona matokeo ya kushtua ya kamati ya pili ya Rais iliyowasilishwa kwa Rais wa Tanzania Mh. Dk John P. Magufuli leo asubuhi ambayo imeangalia nyanja za historia za kiuchumi na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini.

Kamati ya Pili imetoa matokeo yake kwa kutumia matokeo ya Kamati ya Rais ya Kwanza, iliyotangazwa tarehe 24 Mei 2017, ambayo Acacia imeikanusha vikali. Kamati hiyo ilipata matokeo yake kwa kutumia sampuli ya kontena 44. Kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20 tulizonazo ni vigumu kuoanisha matokeo yetu na yaliyokutwa na kamati, na kamati imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10 kuliko thamani halisi ya makanikia

Kamati ya Pili inadai kuwa Acacia imetangaza kiasi cha chini cha mapato kuliko inavyopata na kulipa kodi kidogo kuliko inavyostahili kwa miaka mingi na kuficha mabilioni ya dola ya Marekani. Na hivyo imefanya mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na Acacia kulipa kodi inayodaiwa na mirahaba, kufanya majadiliano upya ya mikataba mikubwa ya uchimbaji madini, umiliki wa Serikali katika migodi, na muendelezo wa marufuku ya kuuza nje.

Acacia inakanusha vikali tuhuma hizi mpya zisizo na ushahidi. Sisi tumefanya biashara zetu kwa utaratibu bora kabisa na kwa kufuata sheria zote za Tanzania. Tunarudia kusema tena tumeweka wazi kila kitu chenye faida tulichokuwa tunazalisha tangia tuanze uchimbaji Tanzania na tumelipa kodi na mirabaha yote inayotakiwa kulipwa, na kwa kuongezea mahesabu yetu tunayotoa yanakaguliwa kila mwaka kwa viwango vya kimataifa vinavyoendana na IFRS.

Acacia kwa muda mrefu tulitaka kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuwa tunaamini wote tuna malengo sawa katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Hata hivyo, ushirikiano huu lazima uwe na misingi ya haki kwa wadau wote, ikiwa ni pamoja na 96% ya wafanyakazi katika migodi yetu ambao ni Watanzania, na wanahisa wetu ambao wamechangia dola bilioni 4 za uwekezaji ambazo Acacia imefanya ndani ya nchi hadi sasa.

Acacia bado inakaribisha mazungumzo na Serikali kuhusu suala hili na inaendelea kutathmini nini inaweza kufanya . Tutatoa taarifa zaidi kwa soko kadri tutakavyoweza kufanya .

VYANZO: Amana Epaphra/ Facebook.

Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

ORODHA YA NCHI ZA KWANZA NA ZA MWISHO KWA AMANI DUNIANI.

Marekani:  Ripoti ya Taasisi ya Uchumi na Amani imepata mataifa kumi tu ulimwenguni ambayo hayapo katika vita na migogoro kabisa. Kwa mujibu wa Ripoti ya Kimataifa ya Amani 2016, Botswana, Chile, Costa Rica, Japan, Mauritius, Panama, Qatar, Uswisi, Uruguay na Vietnam ndio nchi pekee ambazo hazipo kwenye vita wala migogoro yeyote ile ya kuhatarisha amani.. Iceland inaongoza orodha ya nchi zinazoongoza kwa amani ulimwenguni, ikifuatiwa na Denmark, Austria, New Zealand, Ureno, Jamhuri ya Czech, Uswisi, Canada, Japan na Slovenia - wakati Marekani ikiwa kwenye nafasi ya 103. Palestina imepanda kutoka nafasi ya 163 mpaka nafasi ya 148. Syria iliyoharibiwa na vita imewekwa chini ya orodha, chini kuliko Sudan Kusini, Iraq, Afghanistan, Somalia, Yemen, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ukraine, Sudan na Libya. "Ripoti inalinganisha amani duniani kwa kutumia mandhari tatu pana: hali ya utulivu na usalama katika jamii; kiwango cha mgogoro wa ndani au wa kimataifa; na kiwango cha kije...

JAGUAR KUACHIA WIMBO BAADA YA KUAPISHWA MBUNGE.

Mbunge wa Starehe, Kenya, "Jaguar" anajipanga kutoa wimbo mpya mara tu baada ya kuapishwa kua mbunge. Katika chapisho lake la kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Jaguar aliupendekeza wimbo wake wa "Ndoto" kama salamu kwa Wakenya na watu walio nje ya Kenya. Charles Njagua, ambae ni maarufu kwa jina la Jaguar, ana Aliahidi mashabiki wimbo mpya baada ya kuapa rasmi kama mbunge.  Mimbaji huyo ambaye ametoa hits kadhaa lakini sasa anazingatia siasa baada ya kushinda kiti, aliwaambia mashabiki kwenye vyombo vya habari vya kijamii kwamba wimbo mpya, unaitwa "Ndoto", uko tayari na utaachiliwa haraka baada ya kuapa. "Sasa ni karibu miongo miwili tangu mimi kuweka mguu katika studio ya kurekodi,   alisema Jaguar katika chapisho lake. CHANZO: www.tuko.news

KASHFA YA MAPENZI KATI MH.MBOWE NA WEMA SEPETU.

MH.FREEMAN MBOWE AKIWA NA WEMA SEPETU. Siku chache baada ya ile skendo ya ngono iliyosababisha wakili na mshauri wa Chama cha ACT -Wazalendo , Bwana Albert Msando kujiuzulu kwenye nyadhifa yake ya chama ,yameibuka mangine kwenye chama kikuu cha upinzani Tanzania ,CHADEMA ,baada ya kusambaa kwa kipande cha sauti kinachodaiwa kua ni mazungumzo kati ya mwenyekiti wa chama hicho na mbunge wa Hai Mh.Freeman Mbowe na Miss Tanzania 2006 ,mrembo Wema Isack Sepetu. SIKILIZA HIVI VIPANDE VYA SAUTI: Bonyeza hapa chini kusikiliza maongezi hayo yanayodaiwa kuwa ni kati ya Wema Sepetu na Mh.Freeman Mbowe; Bonyeza hapa chini kusikiliza majibu ya Wema Sepetu; Bonyeza hapa chini kusikiliza majibu ya Mh.Freeman Mbowe; VYANZO: Jamii Forums,                   YouTube.com,                   Perfect255.com.                   

"GIGGS HAFAI KUWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA", BABA YAKE ANASEMA...!!!

Ryan Giggs. Chama cha Soka cha Wales (FAW) siku ya jumatatu kilitangaza kumchagua winga wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs kama kocha wa timu yao ya taifa kwa mkataba wa miaka minne. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 44 anachukua kazi iyoachwa na Chris Coleman, ambaye aliiongoza Wales kwenye nusu fainali za Euro 2016 lakini aliacha kazi mwezi Novemba ili kuchukua nafasi ya kuifundisha timu ya Sunderland ya ligi kuu ya Uingereza. Giggs alisema kuwa anajivunia kwa kupewa kazi hiyo na pamoja na changamoto iliyo mbele yake baada ya Wales kushindwa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Urusi na sasa wanazingatia michuano ya Ulaya ya 2020. "Siwezi kusubiri kuanza kufanya kazi na wachezaji tunapojiandaa kwa ajili ya michezo muhimu baadaye mwaka huu," alisema. Lakini baba mzazi wa Giggs, Danny Wilson ana maoni  tofauti sana...!!! Anakiri kwamba mwanae anamtia aibu na anasema hastahili kuchukua kazi hiyo ya ukocha wa timu ya t...

MCHEZAJI WA ZAMANI WA UINGEREZA AMESEMA ALICHEZA NA WACHEZAJI WATATU MASHOGA KWENYE TIMU.

Carl Hoefkens (jezi no.2) alichezea West Bromwich Albion na Stoke City wakati wa enzi zake ligi kuu ya England. Beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza amesema alicheza pamoja na wachezaji wenzake wawili wa mashoga ndani ya timu, na mmoja alikua na jina kubwa. Carl Hoefkens, West Bromwich Albion na Stoke City siku za nyuma, anasema wachezaji hao walikua wazi na hawakujificha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingawa bado hawajulikani kwasababu ya maombi yao wenyewe ya kuomba kutotangazwa. Justin Fashanu, ambaye alijiua mwaka 1998, alikuwa mchezaji wa mwisho wa kazi nchini England kuja nje kama mashoga - mwaka 1990. Hoefkens alipokua (kushoto), alipokua anachezea Stock  City. Hoefkens aliyecheza Uingereza kwa miaka minne, akiondoka mwaka 2009, alidai kuwa mchezaji mwenzake mmoja wa timu alikua anaweza kuja kwenye uwanja wa mafunzo ya klabu na mpenzi wake wa kiume  lakini aliwaomba wenzake kutokuwaambia watu wangine wa nje ya timu. 'Nilicheza pamoja n...

TUPAC SHAKUR ALIBAKWA JELA !!!

             Ulimwengu wa filamu za Hollywood na muziki wa Hip Hop juzi ulipatwa na mshangao baada ya mtayarishaji wa filamu inayohusu maisha ya hayati Tupac Shakur ,L.T Hutton kuelezea sababu zilizomfanya kumbadilisha muongozaji wa filamu hiyo kutoka John Singleton na kumuweka muongozaji Benny "Boom" Douglas.  Filamu hiyo inayoitwa "all eyez on me" tayari imekwisha andaliwa na inatarajiwa kuzinduliwa leo tarehe 16 Juni 2017.       Akizungumza kwenye mahojiano redioni L.T Hutton amewashtusha watu wengi baada ya kudai kwamba walishindwana na muongozaji wa mwanzo bwana John Singleton sababu muongozaji huyo aling'ang'ania kuwepo kwa matukio (scene) ambazo kwa maoni yake zisingependeza.        Matukio ambayo John Singleton alipenda yawepo katika filamu hiyo ni pamoja na kutaka filamu hiyo ianze na scene ya Tupac akilazimisha kumlawiti msichana wa kizungu.!!!          Singleton pia ali...

MOHAMMED DEWJI NA BILL GATES KUTOA NUSU YA UTAJIRI WAO...!!!

MOHAMMED DEWJI AKIWA NA BILL GATES. Mfanyabiashara tajiri namba moja Tanzania (kwa mujibu wa jarida la Forbes) na mmiliki wa makampuni ya METL , Mohammed "Mo" Dewji ,wiki chache zilizopita amekua mmoja wa mabilionea 14 wapya kujiunga katika mpango wa kuchangia misaada kwa jamii uitwao "Giving Pledge".                 Mpango huo ulioanzishwa na familia ya mfanyabiashara tajiri namba moja duniani (kwa mujibu wa jarida la Forbes) na mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill Gates pamoja na rafiki yake bilionea Warren Buffet mwaka 2010, ulikua na tayari umeshaungwa mkono na mabilionea 154 mpaka mwanzo wa mwaka huu (2017). WAASISI WA "GIVIN PLEDGE",WARREN BUFFET, MELINDA GATES NA BILL GATES.         Mohammed Dewji anakua mmoja kati ya matajiri wachache sana kutoka Afrika kama Patrice Motsepe (Afrika Kusini) na Mo Ibrahim (Sudan) kujiunga na kampeni hiyo ambayo nia yake kubwa ni kushawishi watu matajiri kutoa angalau nu...