PATRICIA MEISTER (64). |
Mwanamke mwenye umri wa miaka 64 amesimulia juu ya jinsi alivyotapeliwa dola 100,000 baada ya kupendana na mtu ambaye ambaye hawakuwahi kukutana.
Patricia Meister, kutoka Queensland, Australia alianza uhusiano wa mtandaoni na mtu ambaye alidhani alikuwa mfanyabiashara mwenye umri wa miaka katikati baada ya mtu huyo kumtumiaa ombi la rafiki kwenye Facebook mwaka 2015.
Akizungumza na Daily Mail Australia, mwanamke huyo alifafanua wakati alipopiga kichwa juu ya visigino kwa upendo, kabla ya kugundua mpenzi wake wa Italia aitwaye 'Carlos' alikuwa tapeli wa Nigeria.
Bi Meister alisema mwanamume huyo alionekana kujali na kufuatilia kila kitu cha maisha yake alipokua anapiga simu kila siku.
'Sijawahi kuwa kwenye tovuti za marafiki(dating websites), na nilokua natumia Facebook kwasababu za kibiashara. Kwa hiyo nilipopata ombi la urafiki, nilidhani haiwezi kuwa na madhara yoyote ", Alisema.
'Nadhani wakati ule, nilikua napitia katika kipindi cha maisha yangu ambapo nilihisi nikiwa mpweke. Nilikua sina mume muda mrefu na sijawahi kuwa kwenye mitandao ya urafiki '
'Tulianza kuzungumza. Alikuwa mcheshi, mwenye akili na alionekana kuwa na elimu. Alikuwa mzuri sana kwenye lugha ya Kiingereza na alikuwa yuko kimapenzi sana.
Nilimpenda sana katika hatua hiyo '
Alisema huyo mtu ambaye alidai kuwa alikuwa mjini Brisbane,Australia, alimwambia alikuwa akifanya kazi za ubunifu wa ndani(interior design) na asili yake ilikua ni ya Kiitaliano na Scotland.
Wawili hao walibadilishana ujumbe kila siku kabla ya kuanza mazungumzo katika simu.
'Nilipoisikia sauti yake mara ya kwanza ilikua tofauti na ile niliyoitarajia. Nakumbuka nilipokua najiuliza kuwa ile ni rafudhi gani "...sikuweza kuitambua ilikua ni rafudhi gani'
'Sikuweza kuitambua ile rafudhi kwa wakati huo, lakini nikifikiria kwa sasa, ilikua ni dhahiri kutoka Afrika ... Alikua Mnigeria.'
Licha ya kumtilia baadhi ya mashaka, Bibi Meister aliendelea kuzungumza naye na wiki zilipita.
Ndani ya wiki nane katika uhusiano wao, 'Carlos' alimwomba kama angeweza kumkopesha $ 600 kwa sababu kadi yake ya benki ilikataa kufanya kazi wakati akiwa Malaysia kibiashara.
'Sikuona ni sawa lakini nilifikiri na kuona kuwa sio kiasi kikubwa cha pesa kupoteza". Halikuwa ombi kubwa kwa hiyo nilimtumia, "
'Kiasi fulani nilifikiri ilikuwa ni kosa hivyo nikamwuliza, nikisema "wewe ni mfanyabiashara, kadi yako ya benki lazima ifanye kazi ...!" Hadithi yake bado sikuielewa!'
Lakini kuomba kwake fedha hakukuishia hapo, aliweza kutengeneza sababu kila wakati alipotaka kuomba fedha.
'Carlos' alikuwa akipanga safari ya kurudi nyumbani kwa Brisbane wakati bidhaa zake zikishikiliwa na forodha(customs) ya Malaysia. Na hivyo alikuwa na haja ya kulipia.
'Kiasi cha kwanza nilichomtuma kilikuwa $ 7,000. Alipokwenda kuchukua fedha, aliniambia alikuwa anahitaji $ 7,000 $ nyingine ", Alisema Bibi Meister.
'Kila kitu alichosema kilikua na "nyaraka" - na daima kulikuwa na mwanasheria nyuma wakati tunazungumza kwenye simu.
'Alipojaribu kunilipa, alisema benki yake haiwezi kufanya uhamisho mkubwa wa kimataifa kwa hiyo alipanga kutumia kampuni ya kusafirisha vifurushi ili kunitumia fedha badala yake.'
Bi Meister alisema alipewa kiungo(link) kwenye tovuti na 'karatasi ya kufuatilia', ambako aliweka jicho la karibu juu ya usafirishaji wa kifurushi hicho.
Lakini wakati kifurushi hicho kilopofika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, kulikuwa na ada ya $ 25,000 ya kuruhusu fedha ziondoke nchini.
'Carlos alikuwa ameorodhesha anwani yangu ya biashara kwenye nyaraka, hivyo nilikuwa na wasiwasi kwa kuwa kuna mkoba uliojaa fedha wenye jina langu.
'Kwa wakati huo, nilidhani ninaweza kuonekana muarifu ikiwa nitaruhusu fedha zangu kwa jina langu kukaa pale, nikaona ni vizuri kulipia pesa hiyo ili nipate fedha yangu'.
Bibi Meister alifanya malipo hayo makubwa lakini kifurushi hicho kilipofika uwanja wa ndege wa Melbourne, kilikumbana na ada nyingine.
'Nilikua tayari nimelipa sana.Fedha ilianza kuwa ngumu kupatikana. Alikua amesha chukua kiasi cha mwisho cha pesa zangu,'
,alisema.
Siku iliyopangwa kuwa ndiyo atakayopokea kifurushi cha fedha zake, alipokea simu.
'Nilipokea simu kutoka kwa mtu akisema Carlos na mwanasheria wake wamepata ajali kubwa ya gari hivyo walihitaji fedha kwa gharama za matibabu,'
'Tumbo langu lilishuka mpaka kwenye viatu vyangu... Nilitambua wakati huo kuwa nimesha tapeliwa. '
Bibi Meister hakulipia pesa hizo za matibabu na wawili hao hawakuzungumza kwa karibu wiki.
'Kisha akajaribu kuomba fedha zaidi ili kulipia ada zake za matibabu lakini wakati huo, nilikuwa nimeshatumumia dola yangu ya mwisho,'
,alisema.
'Sikuweza kumlipia tena na hata nikamwambia sitaki kumtumia pesa tena. Muda mfupi baada ya hayo, alipata "ahueni ya ajabu" lakini niliacha kuzungumza naye wakati huo.
Bi Meister alijaribu kutoa ripoti hiyo kwa polisi lakini hawakuwa na kitu ambacho wangeweza kufanya baada ya $100,000 kwa jumla.
Na miezi miwili baadaye, alipokea ujumbe wa maandishi kutoka kwa Carlos, akisema: 'Hii yote ni kutokuelewana.'
Bila kuwaza mara mbili, Bibi Meister alimjibu 'wewe ni tapeli'
Baada ya kumuita tapeli, alimaliza mazungumzo yetu kwakusema: "Nipate kama unaweza, mpendwa wangu",
Bibi Meister alisema hatimaye alipata kikundi cha msaada kinachoitwa Romance Scams ambapo wanawake wanasimulina hadithi zinazofanana na yake.
CHANZO:
dailymail.co.uk

Comments
Post a Comment