Arusha,Tanzania:
Eneo la Mamlaka ya Uhifadhi wa Ngorongoro imeanza kukuza malisho ya virutubisho vya kumlisha na kumtunza Faru Fausta (54).
Hatua hiyo itasaidia kupunguza kiasi cha pesa ambayo hutumika kwa kununua nyasi kutoka Kenya. Faru Fausta anakaa katika mahali maalum katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kama njia ya kumlinda kutoka kushambuliwa na wanyama wengine wa mwitu.
Akizungumza na waandishi wa habari, meneja wa lishe wa NCAA, Bwana Hillary Mushi alisema mamlaka imetenga ekari mbili za kukuza nyasi, ambazo zitakua kwa miezi saba.
Alisema, hatua hiyo inania ya kupunguza gharama ya kumtunza Faru huyo mzee zaidi duniani ambaye amekua miongoni mwa vivutio vikuu vya utalii katika NCAA.
NCAA humlisha Faru Fausta mifuko 250 ya virutubisho yenye thamani ya Shilingi milioni 5 kila baada ya miezi minne.
"Ni hatua nzuri, ambayo inalenga kupunguza gharama za kupata malisho yake ambayo huchukua muda mrefu sana ikiwa ni pamoja na kupata vibali kutoka Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Mamlaka ya Dawa na Chakula ya Tanzania (TFDA) na idara nyingine za serikali," alisema.
Kwa upande wake, mmoja wa wahadhiri katika chuo cha mafunzo ya mifugo ya Tengeru, Oshimu Mollel alisema kuwa malisho hayo yana virutubisho vinavyoukinga mwili wa Faru na magonjwa.
"Vinatokea Marekani na tunaweza kuvuna katika siku 72 ikiwa tutapanda kwenye udongo wenye rutuba," alisema.
Akizungumza juu ya hali ya Faru Fausta, mtaalam wa wanyama wa NCAA, Dk.Athanas Nyaki, alisema kuwa Faru huyo alikuwa kwenye hali nzuri kutokana na usimamizi mzuri wa maafisa wa serikali.
"...amehifadhiwa mahali bora na salama, ni vigumu kwa yeye kushambuliwa na majangili au wanyama wengine wa mwitu," alisema.
Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ni kati ya maeneo madogo ya uhifadhi yenye idadi kubwa ya Vifaru duniani.
Faru hao wanalindwa wakati wote kwa kutumia vifaa maalum.
CHANZO:
allafrica.com
Comments
Post a Comment