Serikali ya Shirikisho la Urusi inadaiwa kuwa tayari kukafanya jaribio la silaha kubwa ya nyuklia "Satan 2" ambayo haitaweza kuzuiwa na ngao zozote za kinyuklia zilizopo katika nchi za magharibi kwa sasa.
Silaha hiyo ilikua ikizungumziwa chini chini sasa inasemekana kuwa tayari kujaribiwa kabla ya mwisho wa mwaka.
Silaha hiyo iliyopewa jina "Satan 2" (Shetani wa pili) na Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi(NATO),ina uwezo wa kuteketeza eneo kubwa sawa na eneo la nchi nzima ya Ufaransa.
Silaha hiyo aina ya ICBM ya tani 100 itachukua vichwa vya nyuklia(Nuclear Warheads) 15 - kila kimoja chenye kasi ya hypersonic ya 4,000mph(Maili elfu nne kwa saa) sawa na Kilomita elfu sita na nusu kwa saa(643.376 Kmph).
Mwaka jana, picha za kwanza za "Shetani wa pili" ambayo jina rasmi la RS-28 Sarmat, zilitolewa.
Sasa, vyombo vya habari vya Serikali ya Urusi vinasema silaha hiyo itafanyiwa jaribio kabla ya mwisho wa 2017.
Wahandisi wa Kremlin wanasema kuwa wanalenga kuifanya Satan 2 tayari kwa vita kabla ya mwisho wa mwaka 2020.
RS-28(Satan 2) itachukua nafasi ya silaha ya sasa ya Urusi ya SS-18, inayoitwa Satans.
Inasemekana kuwa na kasi ambayo hakuna mfumo wa kuzuia wa kombora ya nyuklia unaoweza kukabiliana nayo kwa sasa.
RS-28 itajaribiwa kwenye Cosmodrome ya Plesetsk, kaskazini magharibi ya Urusi, kabla ya mwisho wa mwaka.
Vichwa vya nyuklia 15 vitakavyokua ndani ya "Shetani wa pili" vitakua na nguvu ya 750kt kila kimoja ambayo ni mara 50 zaidi ya bomu lililopigwa Hiroshima.
Uendelezaji wa hivi karibuni wa nyuklia wa Urusi unakuja kama Donald Trump anataka kuongeza silaha za Marekani mara kumi, kulingana na ripoti.
Lakini Trump alikanusha haraka kukataa hii kwenye Twitter,kwa kuandika taarifa kuwa ni "habari bandia".
CHANZO:
dailystar.co.uk
Comments
Post a Comment