Kampuni ya kuchimba madini ya Acacia iliripoti kushuka kwa pato kwa asilimia arobaini(40%) ,kwa robo ya tatu, kama athari ya kupigwa marufuku kusafirisha madini nje na serikali ya Tanzania.
Matokeo ya kampuni ya Acacia kwenye soko la hisa la London (FTSE 250)yalikuwa sawa na matarajio, kutokana na kuwa haikuweza kuuza nje ka karibu asilimia Thelasini(30%) ya mavuno yake tangu Machi kutokana na mgogoro wa kodi na serikali ya Tanzania.
Mapato yalifikia dola 171m (£ 131m) katika miezi mitatu hadi Septemba, wakati mapato kabla ya riba, kodi, kushuka kwa thamani na uhamisho ulipungua kwa asilimia sitini(60%) hadi $ 50m, hasa kutokana na mauzo ya chini.
Msimamo wa pesa(net cash position) wa Acacia ulipungua hadi $ 24m kutoka $ 90.7m mwezi Julai mgogoro ulipoanza.
Mchimbaji huyo alichukua hatua ya kushusha uzalishaji kwenye moja ya migodi yake mitatu nchini Tanzania wakati wa robo, kwa sababu inaonekana kupata hasara kutokana na marufuku ya kuuza nje ya mchanga wa dhahabu.
Serikali ya Tanzania imeshutumu Acacia kwa kutoa taarifa ya chini ya kiasi cha dhahabu inayoiuza nje na inadai kodi pamoja fidia inayofika hadi $ 190bn.
Jana mdau mkubwa wa umiliki wa Acacia, kampuni ya Barrick Gold ilisema kuwa imefanya jaribio la kutatua mgogoro na serikali kwa kuchukua hatua ya kuipa serikali hisa zaidi katika migodi ya Acacia kama utangulizi wa kuondoa marufuku ya kuuza nje.
Acacia pia kulipa dola 300m wakati muswada wake wa kodi unajadiliwa.
Hata hivyo mpango huo utaenda kwa wanahisa wa Acacia kwa idhini. Acacia ilisema hakuna pendekezo rasmi lililowekwa bado na lilikuwa linatafuta "ufafanuzi" juu ya mapendekezo.
"Biashara yetu imeendelea kuwa imara wakati wa changamoto nchini Tanzania," alisema Brad Gordon, Mtendaji mkuu.
Hisa za Acacia zilizoshuka kwa 3.7pc zimeongezeka jana baada ya habari za mkataba huo, kabla ya kuanguka tena baada wawekezaji kutaka maelezo kwa usahihi zaidi.
"Wakati hatua zinaonekana kuwa zimefanyika, bado kuna hali ya kutokua na uhakika, kama inavyothibitishwa na matokeo ya soko kwa habari za jana," alisema machambuzi wa Investec.
CHANZO:
telegraph.co.uk
Comments
Post a Comment