Timu za Arsenal na Manchester City zinakabiriwa na adhabu kwa kuvunja sheria mpya za kubadirisha wachezaji wakati wa mechi za michuano ya kombe la Carabao, Jumanne, 24 Oktoba 2017.
Katika mechi hizo Manchester city iliitoa Wolves kwa penalti, wakati Arsenal ilihitaji muda wa ziada kupata ushindi dhidi ya Norwich kwenye uwanja wa Emirates.
Hata hivyo, vilabu hivyo vyote viwili zinasubiri hukumu ikiwa wamevunja sheria ambayo inaweza kusababisha kutupwa nje ya mashindano hayo.
Vilabu hivyo vyote vya Ligi Kuu vilifanya mabadiliko mara nne, mawili ndani ya dakika tisini na mawili wakati wa muda wa ziada, na tayari zinawekwa kwenye mahitaji ya ufafanuzi wa kama hii inaruhusiwa.
Sheria kwenye michuano ya kombe la Carabao inaruhusu timu kufanya mabadiliko ya wachezaji mara nne, lakini sheria inaeleza kwamba timu zimeruhusiwa kubadirisha mchezaji mmoja tu katika muda wa ziada.
Alipoulizwa ikiwa Arsenal walifanya mabadiliko chini ya kanuni, Kocha Arsene Wenger alijibu: "Ndiyo."
Meja wa Norwich, Daniel Farke aliongeza kwa kusema: "Nadhani sheria zimebadilika lakini bado kuna mkanganyiko."
Adhabu kwa pande zote mbili inaweza kuwa kurudia mechi, au hata mbaya zaidi ya kutolewa kwenye mashindano.
CHANZO:
teamtalk.com
Comments
Post a Comment