Afisa mtendaji mkuu wa benki alifukuzwa kazi na kuchunguzwa na Shirika la Uhalifu wa Taifa baada ya kuweka pauni za Uingereza 350,000 ( £ 350,000 ) pesa taslimu aliyopewa na Mfalme wa Ghana.
Mark Arthur wa benki ya Kimataifa ya Ghana Bigwig aliitwa kwenye nyumba ya Osei Tutu II huko Henley-on-Thames na kupewa £ 200,000 pamoja na $ 200,000 na kuagizwa aiweke kwenye akaunti ya benki ya Mfalme huyo.
Licha ya noti hizo kuwa na namba za mfululizo zinazofuatana (consecutive serial numbers) Bwana Arthur alisema aliona kuwa haifai kumhoji mfalme na kwenda kuiweka benki kwa kutumia usafiri wa teksi ya uber.
Punde baada ya Bwana Arthur kuweka pesa hiyo benki, taarifa ya utakatishaji wa fedha ilifika katika jiji la London, Uingereza na kugharimu ajira yake.
Bwana Arthur alielezea kwenye taarifa yake ya ushahidi kuwa Mfalme alimwambia kwamba pesa hizo zimekusanywa kutoka kwenye akaunti za benki za nchini Ghana na kupelekwa Uingereza.
Pia alidai kwamba Mfale alimpa $ 200,000 ili aitume kwenda kwenye akaunti ya benki ya Standard iliyopo Jersey.
Kufuatia uhamisho huo, alisimamishwa na kufutwa kazi baada ya uchunguzi na wahasibu wa nje wa Grant Thornton.
Kwa mujibu wa benki hiyo ya Ghana, Afisa huyo aliefukuzwa kazi alishindwa kufuata sheria za kuzuia utakatishaji fedha pamoja na kukiuka sera za usalama.
Bwana Arthur, mkurugenzi mtendaji wa benki, anasema kuwa amana na uhamisho huo viliidhinishwa na mtendaji mkuu wa Benki ya Kimataifa ya Ghana, Joseph Mensah.
Bw Mensah hakukubaliana akidai kuwa "hakuwa na hata mamlaka ya kuidhinisha kiasi kikubwa".
Mfalme wa Ghana na mtawala wa Asante hufikiriwa kuwa mfalme tajiri zaidi wa Afrika, akiwa na vitalu vya kuchimba dhahabu na mashamba makubwa ya kakao.
Kwa mujibu wa taarifa yake ya ushahidi, Bwana Arthur alisema kuwa hakuweza kufuata sheria za kupinga kwa sababu ya hadhi ya ufalme.
CHANZO:
dailymail.co.uk
Comments
Post a Comment