Ikiwa umewahi kuchunguza kwa ukaribu zipu kwenye nguo zako nyingi, utakua tayari umeona herufi zinazosomeka "YKK," katika herufi kubwa, kwa mengi yao.Herufi hizi zipo kwenye kila kitu kutoka kwenye nguo za jeans, makoti hata kwenye mabegi.
Herufi hizo zinasimama kwa niaba ya "Yoshida Kogyo Kabushikikaisha" ambayo, kutoka kwenye lugha ya Kijapani, inaelezea "Yoshida Company Limited" yaani "Kampuni ya Yoshida"
Kampuni hii ni ya mtengenezaji wa zipu aitwaye Tadao Yoshida, ambaye aliianzisha mwaka wa 1934. Kwa wastani, kampuni hiyo inatengeneza nusu ya zipu duniani, ambayo ni zaidi ya zipu bilioni 7 kila mwaka.
Kwa uhalisia Yoshida hakua mvumbuzi wa zipu duniani, zipu zilivumbuliwa na Mmarekani, Whitcomb L. Judson, miaka ya 1890.
Kampuni yake sasa ipo, na inabuni na kutengeneza zipu za kisasa ikijulikana kama Talon, Inc. Bidhaa za kampuni hiyo hutumiwa makampuni kama Brooks Brothers na Uniqlo.
Lakini YKK ina sifa isiyofananishika katika sekta ya mitindo. Imeunganishwa kabisa, ambayo ina maana kwamba kampuni inadhibiti kila sehemu ya mchakato wa utengenezaji wa zipu, kutoka kwenye kuchonga chuma ili kutengeneza zipu mpaka kwenye kufungasha zipu zilizokamilishwa.
Kama Seth Stevenson aliandika katika jarida la Slate kwama "YKK hutengeneza zipu zinazotegemewa sana, huwapeleka kwa wakati bila kushindwa, hutengeneza katika rangi, malighafi, na mitindo mbalimbali na kamwe haipatikani kwa bei mbaya."
Kwa sababu ya kuaminika kwake, YKK inajulikana kwa wazalishaji. Tumeona wote ugumu wa kuvunja zipu hizo unaweza kuharibu nguo nzima. Ina maana zaidi kwenda na chapa inayoaminika. Na ndiyo sababu zipu za YKK ziko kila mahali.
CHANZO:
businessinsider.com
Comments
Post a Comment