Mesut Ozil amedaiwa kuwaambia wachezaji wenzake wa timu ya Arsenal kuwa ataondoka kwenye klabu hiyo na kuingia Manchester United.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia anasema ana uhakika kwamba anaweza kuhamia Old Trafford, lakini haijulikani kama United wako tayari kuchangamkia mpango huo kwa mujibu wa John Cross wa gazeti la Mirror,Uingereza.
Mjerumani huyo anamaliza mkataba wake na Arsenal katika kipindi kijacho cha majira ya joto, na hivyo anaweza kuondoka bila gharama yeyote (bure).
Kuelekea Old Trafford kutamfanya Ozil akutane na meneja Jose Mourinho, ambaye anamjua vizuri kutoka wakati wakiwa pamoja Real Madrid.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema hivi karibuni kuwa klabu hiyo inaweza kumuuza Ozil mwezi Januari, ikiwa watashindwa kuongeza mkataba wake wa sasa na klabu, kwa mujibu wa Jeremy Wilson kwenye The Telegraph.
Beki wa zamani wa Arsenal Martin Keown amesema kuwa Ozil tayari amehama Arsenal "kisaikolojia" na anapaswa kuuzwa, kwa mujibu wa BBC 5 Live Sport.
Kwa mujibu wa WhoScored.com, Ozil ameanza michezo minne ya Ligi Kuu ya Arsenal msimu huu na alikuwa kwenye benchi la wachezaji wa akiba katika mechi waliyopoteza Jumamosi 2-1 huko Watford.
Keown pia aliendelea kumlaumu Ozil kuwa ndiye aliyesababisha goli walilofungwa dakika za mwisho kwenye mechi dhidi ya Watford, kwa mujibu wa BT Sport (h / t Dan Ripley kwenye Mail Online).
Wakati akicheza chini ya Mourinho hapo awali kwenye klabu ya Real Madrid , Ozil aliandika kwenye kitabu cha historia yake kuwa waligombana na Mourinho huko Madrid, katika historia yake ambayo ilikuwa ikichapishwa pia katika jarida la Kijerumani la Bild (h / t Sky Sports).
Manchester United wanaonekana kutokua na tatizo la viungo washambuluaji wakiwa na Juan Mata, Jesse Lingard, Henrikh Mkhitaryan na Paul Pogba.
Ozil hajafanya chochote cha kuvutia msimu huu, ingawa Opta alionyesha kile anachoweza kutoa.
SOURCE:
bleacherreport.com
Comments
Post a Comment