RAISI ROBERT MUGABE. |
Wanasayansi wanaoheshimika kutoka chuo kikuu cha Taifa cha sayansi na teknolojia cha nchini Zimbabwe wamekua wakiendesha utafiti kwa miaka mingi kuchunguza kwanini Raisi Robert Mugabe wa nchi hiyo mwenye umri wa miaka 92 hafariki.
Hii ilianza tangu mwaka 1999 ambapo iliwekwa wazi kwamba raisi huyo alikua hajawahi kubadilika sura wala nywele tangu alipoanza kutawala nchi hiyo mwaka 1980.
Raisi Mugabe aliwahi kusikika akisema kwamba haitaji kwenda Gym wala kula mboga za majani ili abaki kua na afya njema sababu alizaliwa ili aishi milele.
Baadhi ya watu walianza kuamini maneno hayo baada ya kuanza kuchunguza picha za raisi huyo na kugundua kwamba hana muonekano tofauti tangu miaka ya sabini mpaka sasa.
Mabilioni ya dola za Kizimbabwe yaliwekezwa katika utafiti huo ambao mwisho umekuja na matokeo kwamba wataalamu hao hawakuona mvunjiko (decay) yoyote katika DNA ya raisi huyo mzee zaidi Afrika.
Watafiti hao walichukua sample za DNA kwenye miswaki, nguo na machanuo ya raisi huyo kwa miaka lakini wamedai kutoona dalili wala udhaifu wowote kwenye DNA yake.
Raisi Mugabe pia aliwahi kusikika akisema kwamba anatembelea fimbo ili kuwa na muonekano tofauti tu,lakini haitumii ili imsaidie kutembea.
Hata hivyo kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha nchi hiyo ,MDC, Bwana Morgan Tsangerai amepinga matokeo ya utafiti huo na kusema Mugabe ni mtu wa kawaida mwenye mwili wenye mifupa na tishu kama watu wangine.
Akitoa matokeo ya utafiti huo kiongozi wa jopo la wanasayansi hao Dk.Bigbrains Kanonyepa amesema kwamba mara ya kwanza hawakuamini baada ya kukuta raisi huyo anamwili imara ambao hawajawai kukutana nao.
Utafiti huo unatarajiwa kuendelea mpaka mwaka 2018 kipindi bajeti yake itakapofika kikomo.
Hii inamaana kwamba Raisi Mugabe atatawala nchi hiyo milele !!!.
Bado hakuna mtu mwenye uwakika kwamba hii ni habari nzuri au mbaya kwa wananchi wa Zimbabwe.
VYANZO:https://zimbabwe-today.com/zimbabwe-scientists-92-year-old-president-mugabe-will-never-die-special-dna/
Comments
Post a Comment