MOHAMMED DEWJI AKIWA NA BILL GATES. |
Mfanyabiashara tajiri namba moja Tanzania (kwa mujibu wa jarida la Forbes) na mmiliki wa makampuni ya METL, Mohammed "Mo" Dewji ,wiki chache zilizopita amekua mmoja wa mabilionea 14 wapya kujiunga katika mpango wa kuchangia misaada kwa jamii uitwao "Giving Pledge".
Mpango huo ulioanzishwa na familia ya mfanyabiashara tajiri namba moja duniani (kwa mujibu wa jarida la Forbes) na mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill Gates pamoja na rafiki yake bilionea Warren Buffet mwaka 2010, ulikua na tayari umeshaungwa mkono na mabilionea 154 mpaka mwanzo wa mwaka huu (2017).
WAASISI WA "GIVIN PLEDGE",WARREN BUFFET, MELINDA GATES NA BILL GATES. |
Mohammed Dewji anakua mmoja kati ya matajiri wachache sana kutoka Afrika kama Patrice Motsepe (Afrika Kusini) na Mo Ibrahim (Sudan) kujiunga na kampeni hiyo ambayo nia yake kubwa ni kushawishi watu matajiri kutoa angalau nusu ya utajiri wao kwenye miradi ya kusaidia jamii masikini.
Kwenye barua yake ya kujiunga na kampeni hiyo, Mo ambae anakadiliwa kua na utajiri wa dola bilioni 1.36 ($1.36 Billio ns) sawa na karibu shilingi za kitanzania trilioni mbili na nusu, aliandika hivi;
"Tangu siku ya kwanza,wazazi wangu walikua kama chombo cha kuanzisha utamaduni wa kujitolea, jukumu langu kama Muislam ni kutoa na kujali wenye maisha duni katika jamii."
"Kwa kutia saini katika ahadi hii,natumaini nitawashawishi watu kama mimi, Waafrika wenzangu na watu wote duniani kutazama kwa jicho la karibu mali wanazohitaji kumiliki kwaajili ya familia zao dhidi ya uwezo wao wa kutoa...."
"Wote tuna wajibu wa kimaadili kama watu wenye uwezo kwenye jamii kutoa..."
"Nitawaacha na maneno machache ya kuwashirikisha makomredi wenzangu,wakati Mungu akikubariki kifedha ,usiongeze kiwango chako cha maisha, ongeza kiwango chako cha kutoa"
UNAWEZA KUSOMA HABARI KAMILI KATIKA LUGHA YA KIINGEREZA KATIKA LINK HIZI ZA VYANZO VYETU:
http://www.cnbc.com/2017/05/31/14-billionaires-signed-bill-gates-and-warren-buffetts-giving-pledge.html
https://www.forbes.com/sites/kerryadolan/2016/07/21/tanzanian-billionaire-mohammed-dewji-joins-gates-buffett-giving-pledge/?s=ChangeTheWorld#5f58aa78187a
Comments
Post a Comment