Msanii wa muziki wa Hip Hop wa Marekani, Calvin Cordozar Broadus.Jr. maarufu kama Snoop Dogg amethibitisha kuwa anataka kuhamia Uganda baada ya rais wa Marekani, Donald Trump kudaiwa kuziita nchi za Afrika 'Shimo la Choo'.
Snoop Doggy Dogg pia ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki, mtangazaji katika televisheni, na mwigizaji wa filamu ambaye alianza kupata umaarufu mkubwa katika muziki mwaka 1992 wakati alipogunduliwa na mtayarishaji Dr.Dre, na kushiriki katika nyimbo za Dr.Dre kama "Deep Cover", na kisha kwenye albamu ya kwanza ya Dr.Dre, 'The Chronic'.
Kwa sasa tayari ameshauza albamu zaidi ya milioni 23 nchini Marekani na albamu milioni 35 duniani kote.
Mmarekani huyo mweusi mwenye miaka 46 wa ambaye anajulikana kwa nyimbo zake za maarufu kama; The next episode, Drop it like it’s hot, beautiful, Lay low, nk Juzi alirekodi kipande cha video na kukisambaza akisema kuwa anataka kuhamia chini Uganda.
Tazama Video hapa chini:
(TAHADHALI YA MANENO MAKALI YALIYOZUNGUMZWA KATIKA LUGHA YA KIINGEREZA):
Comments
Post a Comment