Wakuu wa afya wanajaribu sana kuangamiza maafa ugonjwa wa Tauni ya hewa(Airborne Plague) huko Madagascar ambayo yamesababisha onyo katika nchi tisa nyingine za jirani.
Zaidi ya kesi 1,300 sasa zimeripotiwa nchini Madagascar, wataalamu wa afya wamebainisha kama mataifa ya karibu wamewekwa kwenye tahadhari.
Ugonjwa huo unaosababishwa na bakteria yuleyule aliesababisha vifo vya watu milioni 50 balani Ulaya katika miaka ya 1300.
Mlipuko huo unasafiri haraka, na maeneo kadhaa sasa yanaonekana kuwa hatari ya kuenea kwa janga, ikiwa ni pamoja na visiwa vya Shelisheli, Afrika Kusini na Reunion.
Msumbiji, Tanzania, Kenya, Ethiopia, Comoros na Mauritius ni nchi nyingine sita ambazo zimepokea tahadhari.
Imearipotiwa kuwa wafanyakazi wa misaada 50 wanaaminika kuwa miongoni mwa watu walioambukizwa.
Tawi la Afrika la Shirika la Afya Duniani(WHO) linasema watu 93 wamepoteza maisha yao kwa ugonjwa huo hadi sasa, chini kuliko 124 iliyoelezwa katika takwimu rasmi za Umoja wa Mataifa.
Afisa wa WHO alisema: 'Hatari ya kuenea kwa ugonjwa huo ni ya juu kwa ngazi ya kitaifa ... kwa sababu iko katika miji kadhaa na hii ni mwanzo wa kusambaa zaidi.'
Taarifa hiyo ya WHO ilikiri kuwa kuzuka kwa ugonjwa huo katika miji tofauti ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Antananarivo - kuongeza hatari ya kuenea.
CHANZO:
dailymail.co.uk
Viongozi wanazidi kuwa na wasiwasi kama karibu theluthi mbili za matukio ya maambukizi huenea kupitia kukohoa, kipiga chafya (hewa) au kwa njia ya mate.
Mashirika ya kimataifa mpaka sasa yametuma zaidi ya dozi milioni moja za dawa za antibiotics kwa Madagascar. Pamoja na karibu vikaragosi 20,000 vya kupumulia.
Hata hivyo, WHO inashauri juu ya vikwazo vya kusafiri au biashara na imeshaomba $ 5.5 milioni (£ 4.2m) ili kupambana na mlipuko wa ugonjwa huo.
Seychelles Air, moja ya ndege kuu za Madagascar, imesimama kuruka mapema kwa mwezi huu ili kujaribu na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
CHANZO:
dailymail.co.uk
Comments
Post a Comment