Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na mke wake wamewekwa kizuizini baada ya mapigano ya usiku wa kuamkia leo.Ripoti zinasema jeshi la nchi hiyo limechukua udhibiti wa mitaa ya mji mkuu na vituo vya televisheni.
Taarifa kwamba ameondolewa kutoka madarakani zinaonyesha kuwa huo ndio mwisho wa utawala wa miaka 37 wa mwanamapinduzi huyo mwenye miaka 93.
Jeshi la nchi hiyo limethibitisha asubuhi hii kuwa mugabe na familia yake wamewekwa kizuizini katika kile ambacho waangalizi wa kimataifa wanakiona kama ni mapinduzi ya kijeshi kutokana na uvumi kwamba makamu wa rais Mugabe aliyefukuzwa wiki iliyopita amerejea kuchukua madaraka ya nchi hiyo.
Vikosi vingine vya usalama vimetakiwa "kushirikiana kwa manufaa ya nchi" na jeshi ambalo limeonya kwamba "kusita kufanya hivyo kwa yoyote kutakabiliwa na majibu sahihi".
Vifaru vya kijeshi vipo kwenye barabara za Harare (Image: Media Barcroft) |
Bado hakuna ripoti zilizohakikishwa kuwa mawaziri na watu wengine maarufu wa serikali hiyo wamekamatwa au "wamekimbia".
Mashirika ya vyombo vy habari ambayo yameweza kupata habari nje ya ripoti ya mji mkuu kuwa kulikua na "machafuko" usiku na milipuko mikubwa takribani mitatu na milio ya risasi za kawaida zilisikika lakini jeshi linatamka kile kilichotokea kama "kuzuia matumizi mabaya ya madaraka bila kumwaga damu."
Jeshi limeonekana kwenye Runinga ya Taifa baada ya kuchukua udhibiti wa vyombo vya habari vya serikali (Image: REUTERS) |
Kumeonekana foleni kubwa katika mashine za kutolea fedha(ATM) watu wengi wakionekana kujaribu kuondoa pesa kutoka kwenye mabenki katika mji mkuu wa nchi hiyo, Harare.
Baada ya kusimamia Shirika la Utangazaji wa Zimbabwe, jeshi lilisema asubuhi hii kwamba jeshi linalenga "wahalifu" walio karibu na Rais Mugabe.
Hakuna neno rasmi juu ya wapi Mugabe mwenye umri wa miaka 93 na mke wake Grace, mwenye umri wa miaka 52, ambaye alieleweka kuwa na nia ya kuchukua nafasi ya urais baada ya kifo chake.
Watu wamejaa katika mabenki na mashine za kutolea fedha kwa nia ya kuondoa fedha (Image: REUTERS) |
Katika taarifa rasmi ya msemaji wa jeshi alisema: "Usalama wao umehakishwa.
"Tunataka kuweka wazi kuwa hii sio mapinduzi ya kijeshi.
"Tunawalenga wahalifu wa karibu na rais (Mugabe) ambao wanafanya uhalifu ambao husababisha mateso ya kijamii na kiuchumi nchini ili kuwaleta mbele ya sheria."
Msemaji huyo aliongeza kuwa "tukimaliza kazi yetu, tunatarajia kwamba hali itarudi kama kawaida".
Msemaji wa jeshi pia aliwataka viongozi wa makanisa kuliombea taifa hilo.
Taarifa pia iliamuru wafanyakazi wote wa jeshi kurudi kwenye makambi mara moja.
mugabe go to the hell,coz umeongoz xana na unauchu wa madaraka.
ReplyDelete