Mmiliki wa timu ya Chelsea ya ligi kuu ya Uingereza, Roman Abramovich tayari ameamua kumtimua kocha Antonio Conte na anazingatia uteuzi wa pili wa Chelsea, kulingana na ripoti nchini Hispania.
Kwa mujibu wa ripoti ya Marca inasema kuwa uhusiano wa kocha huyo kutoka Italia a uongozi wa Chelsea umeshuka "," hawezi tena kuzungumza na mmiliki huyo bilionea wa klabu na mawasiliano yote sasa yanafanywa kupitia kwa Marina Granovskaia, mkurugenzi ambaye anacheza sehemu kubwa katika biashara ya uhamisho wachezaji wa timu.
Ripoti hiyo inaonyesha kwamba matatizo kati ya Conte na Abramovich yalianza kushika kasi tangu kocha huyo alivyoendesha mchakato wa kuamua hatma ya mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Diego Costa wakati wa majira ya joto.
Abramovich anadaiwa kuchukulia vitendo vya Conte ni vya kukosa heshima baada ya meneja huyo wa Chelsea kutuma ujumbe wa maandishi kwa mshambuliaji huyo wa zamani akimwambia kuwa hakuwa sehemu ya mipango yake ya kikosi cha kwanza.
Ripoti hiyo inadai kwamba mchakato wa kumtafuta mrithi wa Conte tayari umeanza na kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 anajua mipango ya Chelsea.
Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa Conte 'anajitahidi kuboresha uhusiano' na wachezaji wa Chelsea na kulikuwa na mvutano wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Watford na Roma.
Conte ana nia ya kuirudisha Chelsea kwenye mbio za ubingwa ingawa timu hiyo tayari iko pointi tisa nyuma ya viongozi wa Ligi Kuu ya Manchester City.
Conte alisaini mkataba mpya na Chelsea mwezi Julai baada ya kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu wake wa kwanza Stamford Bridge, lakini mkataba mpya haufiki katika majira ya joto ya msimu wa 2019.
CHANZO:
Comments
Post a Comment