Makamu wa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameondolewa kwenye nafasi yake, serikali ya nchi hiyo imetangaza.
Bwana Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 75, ameonyesha "sifa za usaliti", Waziri wa Habari Simon Khaya Moyo alisema.
Kuondolewa kwake kunafanya uwezekano mkubwa kwamba mke wa Rais Robert Mugabe Grace atakufuata nyayo za mumewe kama kiongozi wa Zimbabwe.
"Mwelekeo wa Mr Mnangagwa katika kutekeleza majukumu yake ni kinyume na majukumu yake" alisema waziri wa habari.
"Makamu wa Rais ameonyesha sifa za udhalimu."
Bwana Mnangagwa, mkuu wa zamani wa intelijensia, alikuwa mgombea wa anaeongoza katika mchakato wa kumpata mrithi wa Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93.
Kufukuzwa kwa Mnangagwa kunamaanisha mke wa rais Mugabe, Bibi Grace Mugabe anatarajiwa kuteuliwa Makamu wa Rais katika mkutano maalum wa chama cha Zanu-PF mwezi ujao.
Akizungumza na wanachama wa vikundi vya kanisa za asili katika mkutano mkuu wa mji mkuu, Harare, Jumapili, Bibi Mugabe alisema:
"Nyoka lazima apigwe kichwani.
"Tunapaswa kushughulika na nyoka halisi nyuma ya vikundi vinavyopingana katika chama. Tunakwenda kwenye mkutano wa congress kama chama cha umoja."
Mwezi uliopita,Bibi Mugabe alionya kuhusu mipango ya kuipindua serikali, akisema kwamba wafuasi wa Mnangagwa walikuwa nyuma ya njama ya hizo.
Mnangagwa amefanya kazi kwa karibu na Rais Mugabe kwa zaidi ya miaka 40, akiwa msaidizi wake maalum wakati wa vita vya ukombozi mwaka 1977.
Jina lake la utani katika chama ilikuwa "mamba", kwa sababu ya ujanja wake. Bado, hajazungumza kuhusu kufukuzwa kwake.
Bibi Mugabe ambae ni kuu wa ligi ya wanawake wa chama tawala cha Zanu-PF na Mnangagwa wameonekana kama wanaongoza katika mbio za kurithi kiti cha Rais Mugabe kama akifa au akiachia madaraka.
Mugabe madarakani nchini Zimbabwe tangu 1980. Alichaguliwa rais mwaka 1987, akiwa amekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo hapo awali. Anapanga kugombania tena urais katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Mapema, ligi ya vijana ya chama cha Zanu-PF ilimwomba Rais Mugabe kumfukuza Mnangagwa na kumchagua Grace Mugabe.
Hata hivyo, hatua ya kumteua Bibi Mugabe kama naibu wa mume wake katika serikali imeshutumiwa na Mbunge wa upinzani aliyeongoza.
CHANZO:
bbc.com
Comments
Post a Comment