Robinho amehukumiwa miaka tisa jela na mahakama ya Italia baada ya kupatikana na hatia ya unyanyasaji wa kijinsia.
Tukio hilo lililofanyika Januari 2013 wakati nyota huyo wa Brazil alipokuwa akichezea timu ya AC Milan.
Robinho, pamoja na watu wengine watano, wamepatikana na hatia ya kumdhalilisha mwanamke mwenye umri wa miaka 22 katika klabu ya usiku huko Milan.
Kwa mujibu wa gazeti la 'Gazzetta dello Sport' taarifa hiyo inasema kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City ni mmoja kati ya kundi la watu watano ambalo lilipatikana na hatia ya kushambulia kijinsia msichana wa Kialbania katika klabu ya usiku jijini Milan, Italia mnamo Januari 22, 2013.
Mchezaji wa zamani wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil sasa anachezea Atletico Mineiro nyumbani kwao nchini Brazil.
Robinho mwenye umri wa miaka 33 alikuwa akichezea timu ya Rossoneri wakati wa tukio hilo.
Robinho alihamia Ulaya akiwa kwenye kiwango kikubwa kisoka mwaka 2005 na kujiunga Real Madrid kutoka Santos ya Brazil.
Hata hivyo Robinho hakuweza kudumu muda mrefu balani Ulaya baada kushindwa kuonesha kiwango cha kuridhisha.
CHANZO:
metro.co.uk

Comments
Post a Comment