Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika Kusini, afisa mkuu wa chama chake cha MDC amesema.
Bw Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 65, aliyekuwa waziri mkuu, alilipotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na saratani ya koloni.
"Amefariki jioni hii, familia yake imenitaarifu"
Makamu wa Rais wa MDC, Elias Mudzuri aliliambia shirika la habari la Uingereza, Reuters.
Morgan Tsvangirai alizaliwa mnamo Machi 10, 1952 huko Gutu, Zimbabwe. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa mgodi, fundi, na mkulima. Alihudhuria Shule ya Msingi ya Guco ya St. Marks. Kisha alihamishiwa Shule ya Msingi ya Chikara Gutu. Kwa elimu yake ya sekondari, alihudhuria Shule ya High Gokomere.
Alikuwa waziri mkuu katika serikali ya mseto ya Zimbabwe tangu 2009 hadi 2013.
Katika kazi yake ya awali alionekana kuwa mfanyakazi mwenye bidii sana na alifanya kazi katika mgodi wa madini ya nickel( kwa zaidi ya muongo mmoja. Alipanda cheo haraka kutambuliwa na akainuka katika safu ya Umoja wa Wafanyakazi wa Migodi na hatimaye kuwa katibu mkuu.
Tsvangirai alipitia mapambano ya muda mrefu ya kisiasa dhidi ya Rais wa zamani Robert Mugabe.
Alipigwa na kufungwa mara nyingi.
Ugonjwa wa Tsvangirai umesemekana kuwa ulikigawanya chama chake cha MDC (Movement for Democratic Change), na baadhi ya viongozi wa chama hicho waliripoti kuwa wanapambana kurithi kiti cha mwanaharakati huyo wa zamani wa chama cha wafanyakazi.
Comments
Post a Comment