Pichani ni waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau (kushoto), na Rais wa zamani wa Cuba, Hayati Fidel Castro (kulia). |
Maelezo yaliyoandikwa na mtoto wa kwanza wa rais wa zamani wa Cuba , Fidel Castro, kabla ya kujiua yamelishtua taifa la Cuba wiki hii.
Maelezo hayo yaliyoandikwa na mtoto huyo mkubwa wa mwanamapinduzi na rais wa zamani wa nchi hiyo yalikuwa ya kushangaza baada ya kuwa na madai ya kuwa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ni mtoto wa nje wa baba yake marehemu Fidel Castro.
Maelezo hayo yaliyoandikwa kwa mkono na mtoto huyo wa Fidel Castro aliyejiua siku chache zilizopita kwa msongo wa mawazo, Fidel Castro Diaz-Balart, aliyekuwa na umri wa miaka 68, yalionekana kuthibitisha uvumi wa muda mrefu nchini Cuba kwamba Fidel Castro ni baba wa damu wa waziri mkuu wa sasa wa Canada, Justin Trudeau ikiwa ni matokeo ya uhusiano wa siri wa kimapenzi na mke wa mwanasiasa maarufu wa Canada, Pierre Trudeau, Margaret Trudeau mwaka 1970.
Kifo cha mwanasayansi wa nyuklia wa taifa hilo maarufu kama "Fidelito", au Little Fidel(Fidel mdogo) kwa sababu ya kufanana sana na baba yake kimuonekano, kililishangaza taifa hilo kwa maamuzi hayo ya kujiua na maneno aliyoyaacha yamezidi kuwaduwaza wananchi wa Cuba kwa madai hayo kuhusu waziri mkuu wa moja kati ya mataifa makubwa zaidi duniani, Canada.
Katikati ya malalamiko makubwa, maandishi yanasema Fidelito alikasishwa na baba yake marehemu Fidel Castro.
Fidelito aliandika kwamba baba yake, Fidel Castro,
"alikuwa akinilinganisha mimi na Justin kimafanikio" na "kupuuza mafanikio yangu kwa kuyalinganisha na mafanikio yake(Justin Trudeau) huko Canada. "
"Lakini nilipaswa kufanya nini? Mimi ni raia wa Cuba. Ndugu yangu ni raia wa Canada. Ikiwa alizaliwa na kukulia Cuba, angekuwa ameishi katika kivuli cha baba yetu milele kama mimi. "
Wakati Justin Trudeau anajulikana sana kama mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Canada, Pierre Trudeau, picha za kulinganisha za Pierre, Justin na Fidel zinaonyesha kunaweza kuwa na kitu kwenye madai ya watu wa Cuba.
KWENYE PICHA HIZI, KUSHOTO NI PIERRE TRUDEAU,
KATIKATI NI JUSTIN TRUDEAU
NA KULIA NI MAREHEMU FIDEL CASTRO:
Mbali na kufanana kimwili madai hayo yanekuwa yakiungwa mkono na ukweli wa kihistoria.
Wakati mahali alipozaliwa Justin Trudeau, Ottawa, nchini Canada kunaweza kuwa mbali kutoka Havana, Cuba, mama yake Margaret Trudeau alitembelea Cuba miezi tisa kabla Justin kuzaliwa, na kuna picha za kujihusisha na Fidel Castro.
Margaret Trudeau na Fidel Castro jijini Havana, Cuba, miezi tisa kabla Justin kuzaliwa. |
Kulingana na gazeti la Canada la Globe And Mail, Pierre Trudeau na mkewe Margaret walisafiri kwenda Havana na wakawa marafiki wa karibu na rais wa Cuba.
"Njia za Pierre Trudeau na Fidel Castro zilivuka kwa mara ya kwanza mwaka 1970," inasema ripoti ya Globe, kabla ya kuelezea kuwa wanafamilia hao walikuwa na wakati mzuri sana kwenye kisiwa hicho cha Caribbean kuwa "urafiki wa kudumu kati ya arch-liberal Pierre Trudeau na Marxist-revolutionary Fidel Castro.
Margaret Trudeau pia alirejea Cuba mara tu baada ya Justin kuzaliwa. |
Kabla ya kuishagaza Canada kwa kuolewa na Waziri Mkuu wa Canada, mama ya waziri mkuu huyo wa sasa wa Canada ,Margaret alikuwa maarufu katika miaka ya 1970 kwa kashfa za mahusiano ya kimapenzi na watu mbalimbali.
Akiwa kama mtumiaji wa madawa ya kulevya aliyewahi kukiri mwenyewe hadharani, Margaret aliwahi kukamatwa na madawa ya kulevya aliyoweka katika begi la mumewe wakati wakiwa safarini.
Margaret pia na aliwahi kuonekana akiwa amevaa nusu utupu katika ukumbi maarufu wa usiku unaojulikana kama Studio 54, na bado picha hizo zinachapishwa sana kwenye mtandao wa intaneti.
Margaret Trudeau anafahamika sana linapokuja katika kashfa za ngono na wanaume matajiri na wenye madaraka.
Akielezea mahusiano yake ya mwaka 1974 na Ted Kennedy, Margaret Trudeau aliandika katika kumbukumbu yake kuhusu wakati alipokutana na Seneta huyo wa Marekani katika chakula cha jioni nchini New York:
"Hiyo jioni hiyo nilijisikia kuvutiwa nae na sikuweza kukaa karibu na mume wangu kwa mita kadhaa. Pierre(mumewe) hakupendezwa. "
Margaret kisha alihamia kwa mpiga gitaa wa bendi maarufu ya Uingereza ya Rolling Stones 'Ronnie Wood na kisha kuhamia kwa muimbaji wake, Mick Jagger mwaka 1977.
Magazeti ya udaku ya Uingereza yakiwa yamechapisha habari kuhusu kashfa za Margaret Trudeau na wanamuziki wa bendi ya Rolling Stones, mwishoni mwa miaka ya sabini. |
Kashfa hiyo ilipelekea ugomvi na mwisho wa ndoa yake na Pierre Trudeau.
Mwanasiasa huyo wa siasa za kiliberali alishinda katika vita ya mahakama kubaki na watoto peke yake, na akakataa kulipa msaada wowote kwa mke.
Mwanasiasa huyo wa siasa za kiliberali alishinda katika vita ya mahakama kubaki na watoto peke yake, na akakataa kulipa msaada wowote kwa mke.
CHANZO:
yournewswire.
Comments
Post a Comment