Waigaji wa Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un walikua wakihubiri amani katika sherehe za uzinduzi wa michezo ya Olympiki kwa majira ya baridi(Winter Olympic) jijini Pyeong Chang, Korea ya Kaskazini kabla ya kutolewa nje na wanausalama.
Watu hao walionekana kwa muda mfupi katika jukwaa la uwanja huo mkuu wa Pyeongchang, Korea Kusini ili kuwasalimu watu.
Waigaji hao ambao wote walikataa kutoa majina yao halisi - walikuja kwenye sherehe ya ufunguzi -
"kuonyesha dunia, hii ndio amani inaweza kuonekana kama viongozi hao wawili watakapokutana,"
alisema Kim bandia.
Trump bandia alimwiga Rais Trump kwa kuvaa kofia nyekundu ya mpira wa magongo (baseball), lakini ikiwa imeandikwa "USA" sio "Make America Great again"(Unda Amerika Kuu tena)
kauli mbiu ambayo mara nyingi huandikwa kwenye mavazi na matangazo ya Trump.
Pia alivaa tai ndefu ya rangi nyekundu kama ambavyo rais Trump mwenyewe hupendelea kuvaa.
Kim Jong-Un bandia alikuwa amevaa miwani yenye flemu nyeusi akiwa na mtindo wa nywele unaofanana na Kim Jong-Un halisi.
Wakati akitolewa nje, aliuliza hivi:
"Dada yangu naye alitendewa kama hivi?"
Dada wa kiongozi wa Korea ya Kaskazini, Kim Yo Jong, amekuwa mwanafamilia wa kwanza wa familia yao kuweka mguu Korea ya Kusini tangu Vita ya Korea ilipomalizika mwaka wa 1953.
Dada huyo wa kiongozi "mtata" alikuwepo kwa ajili ya sherehe ya ufunguzi wa michezo hiyo ambayo ilishuhudia timu za Kikorea zikiingia chini ya bendera umoja.
Kiuhalisia, mvutano kati ya Pyongyang na Washington unaendelea kuongezeka.
Korea ya Kaskazini inaendelea kuendeleza mpango wake wa silaha za nyuklia licha ya kuwekewa vikwazo vingi vikali kenye kuingiza bidhaa za mafuta, nguo na vyakula vya baharini kutoka Umoja wa Mataifa na Marekani.
Viongozi hao wote wawili, Kim Jong-Un wa Korea ya Kaskazini na Donald Trump wa Marekani wamekuwa wakitupiana matusi na vitisho hadharani.
Kwa jitihada za kuzuia machafuko, viongozi wote Marekani na Korea ya Kusini walikubali kusimamisha mazoezi ya kijeshi katika kanda kwa muda ambao michezo ya Olimpiki itakua ikiendelea nchini Korea ya Kusini.
Aiseeee, hawa jamaa nomaaa!😂😂😂 Mwanzoni nilijua ni real Kim & Trump ati😁😁😁
ReplyDelete