Kila mwaka wakati wa msimu wa majira ya joto, tamasha la kula mbwa linafanyika Yulin, jiji lililo katika jimbo la kusini mwa China la Guangxi.
Tukio la mwaka jana lilimalizika na utata usio wa kawaida. Picha za mbwa wakichinjwa kikatili na kukaangwa zilisababisha gumzo kubwa ulimwenguni kote.
Tamasha la Nyama ya Mbwa la Jinhua Hutou, kama linavyoitwa, lilifungwa ghafla wiki chache zilizopita. |
Wanaharakati wa haki za wanyama na wabunge wa Marekani walitaka Uchina kupiga marufuku kula na mbwa na paka, kama vile Taiwan alivyofanya mwaka 2017.
Serikali za mitaa za Yulin zilichukua hatua za kuzuia na kuficha baadhi ya shughuli za baadhi ya shughuli hizo kama vile kuuza mbwa katika masoko ya chakula.
Hata hivyo, tamasha hilo lilifanyika na kufana zaidi ya miaka mingine.
Kwa nini tabia hii isiyo ya kawaida kwa nchi nyingine imekuwa maarufu sana nchini China?
Nyama ya mbwa haijawahi kuwa kitu cha kawaida katika chakula cha Kichina.
Tofauti na sehemu nyingine ulimwenguni, kula nyama ya mbwa hakujawahi kuwa haramu, lakini tabia hiyo inaoneka kuwa sio maarufu katika siku za nyuma ukilinganisha na sasa.
Kwa mujibu wa Guo Peng kutoka Chuo Kikuu cha Shandong, mmoja kati ya watu wachache ambao walifanya utafiti kuhusu soko la nyama ya mbwa, ni Wachina wachache wenye asili ya Kikorea hula mbwa karibu kila siku kama chakula cha kawaida.
Anasema idadi kubwa ya watu wa kabila kubwa la Han, wanaiona kama chakula cha dawa, ambacho kinaaminika kuupa mwili joto kwa wakati wa majira ya baridi na kuupa mwili baridi wakati wa majira ya joto.
Bio Guo anasema, watu wengi wamekula mbwa agalau mara moja kwa mwaka, ikiwa ni sawa.
Kulingana na utafiti uliofanywa mwaka 2016 na Dataway Horizon, kampuni ya kupigia kura, na Shirika la Ustawi wa Wanyama wa Mifugo, Shirika lisilo la kiserikali la China, karibu asilimia 70 ya watu wa China wanasema hawajawahi kula mbwa. Kati yao, wengi wanasema walifanya hivyo kwa ajali wakati walipo alikwa kwenye chakula cha jioni au kwenye mikusanyiko mingine ya kijamii kama sherehe na kadharika.
Kwa nini tamasha la Yulin limejaa? Na kwa nini migahawa katika miji mingi hujaribu kuweka mbwa kwenye orodha? Jibu ni neno moja ni: uhalifu.
Nyama ya mbwa, kama vile madawa ya kulevya, imekuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa wahalifu.
Kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita Bio Guo amekuwa akienda kutoka kijiji hadi kijiji katika jimbo la Shandong, pwani ya mashariki, akiwauliza wenyeji kile kilichokuwa kinachotokea kwa wanyama wao. Katika kijiji kimoja wanakijiji walimwambia kuwa theluthi moja ya mbwa wao waliibiwa kati ya 2007 na 2011.
Pia aligundua kuwa wawindaji wamekuwa wakipita vijijini na magari wakiua mbwa na mishale yenye sumu na kuwauza kwa watu wa kati(madalali).
Wawindaji wanapata Yuan 10 ($ 1.30) kwa kilo ya nyama, hivyo mbwa wa ukubwa wa kati anaweza kuwa na thamani ya Yuan 70-80 sawa na takribani dola 7 mpaka 8 za kimarekani.
Kijana mmoja wa kiume ambaye alihojiwa naye alikuwa akiwinda ili aweze kupata mapato aweze kuoa.
CHANZO:
Economist Asia.
Comments
Post a Comment