Huu ndio utakaokuwa muonekano wa vyumba hivyo kwa ndani. Picha: Mariot International. |
Kama sehemu ya mpango wa miaka mingi ya Bayern na kampuni kubwa ya hoteli za Mariot na Courtyard, mashabiki hivi karibuni wataweza kupata fursa ya kukaa katika vyumba ambavyo vina dirisha linaloangalia uwanja wa Alianz Arena moja kwa moja.
Vyumba hivyo vya kifahari vya kulala vitakuwa na kitanda cha kikubwa na seti ya televisheni - tu ikiwa umechoka na hat-trick za Robert Lewandowski.
Pia kutakuwa na mahali pa moto ambayo ni maalumu kwa siku za mechi kwenye majira ya baridi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alisema:
"Tunafurahia bidhaa mbili zinazoongoza kama hoteli Courtyard zinazomilikiwa na kampuni ya Marriott na FC Bayern kuingia katika ushirikiano huu wa muda mrefu kibiashara.
"Tunapendezwa na bidhaa mbili zinazoongoza kama Courtyard na Marriott na FC Bayern kuingia katika ushirikiano wa muda mrefu,"
"Kutokana na kwamba Marriott International ni kampuni kubwa zaidi ya hoteli duniani na FC Bayern ni mojawapo ya klabu za soka zenye mafanikio zaidi duniani, ninaamini kwamba huu ni muungano kamili wenye ushirikiano halisi.
"Ninafurahi sana kwamba mashabiki wetu pia wanaweza kufaidika na ushirikiano huu wetu mpya na mshirika wetu wa hoteli atakayetoa huduma za kuvutia kwa mechi zote za nyumbani na ugenini."
CHANZO:
Comments
Post a Comment