Medellín (Colombia) (AFP):
Katika saluni yake ya nywele, Yamile Zapata anatumia faida ya ziara ya Papa Francis ili kuuza pete za funguo zenye picha ya kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani. Lakini anadai sio ambapo pesa halisi iko kwenye mji wa Medellin nchini Colombia.
Zawadi nyingi anazouza katika mji huu wa Colombia hubeba uso wa "mtakatifu" na shujaa wake mwenyewe: Pablo Escobar.
Wakati Francis alikuwa akihudumia na kufundisha kama kuhani wa Yesuit katika miaka ya 1980, Escobar alikuwa akiua mamia ya watu na kufanya biashara ya madawa ya kulevya ya mabilioni ya dola za kimarekani.
"Kila mtu anataka picha za papa sasa, lakini picha za Pablo zinauzika vizuri zaidi," ,alisema Zapata, mwenye umri wa miaka 34, wakati ambao jiji hilo limeandaliwa kwa ajili ya mkutano wa Papa Francis wa wazi siku ya Jumamosi.
PETE ZA FUNGUO ZENYE PICHA ZA PAPA FRANCIS NA PABLO ESCOBAR ZIKIWA ZINAUZWA KWENYE MITAA YA JIJI LA MEDELIN, COLOMBIA. |
Francis alitoa maneno ya huruma kwa waathirika wa vurugu zinazohusiana na madawa ya kulevya jijini Medellin, Lakini licha ya yote, watu wengine huko Medellin humkumbuka Escobar kwa upendo.
"Ninaamini tu kwa Mungu, lakini kile ninachofanya kinaonyesha mema ambayo Pablo alifanya," Zapata alisema.
"Watu katika mji huu hawazungumzi juu ya mambo mabaya, kwa sababu hapa kila mtu anampenda."
WILAYA YA PABLO ESCOBAR;
Mamlaka zilimsaka na kumuua Pablo Escobar mwaka 1993 na kukomesha kile kilichokuwa ni mamlaka kubwa ya madawa ya kulevya ulimwenguni.
Lakini kwa watu wanaoishi katika nyumba ambazo alijenga katika wilaya ya Katoliki ya Medellin katika miaka ya 1980, ilikuwa zaidi kama ufalme wa mbinguni.
Katika jirani ya Yamile, Escobar alijenga nyumba 260 kwa wakazi wa makaazi katika miaka ya 1980. Makazi hayo sasa yameongezeka na kufikia nyumba 6,000.
"Karibu kwenye wilaya ya Pablo Escobar, hapa tunaishi na kupumua amani" ,
ndio maneno yanayosomeka katika bango wakati unaingia katika eneo hilo yakiwa na sura yake.
Sasa ni zaidi ya miongo miwili imepita tangu polisi walipompiga risasi na kumuua Escobar kwenye dari ya jijini Medellin kwa msaada kutoka kwa mamlaka za Marekani.
Hata hivyo bado Pablo ameendelea kua kivutio kwa watu kiasi cha kuendelea kuzungumzwa na kuigizwa kwenye mfululizo wa televisheni, filamu na vitabu vingi.
Mbali na kutengeneza nywele, Zapata huuza vikombe na t-shirt za "Pablo."
Tangu alipobadilisha jina la saluni yake na kuiita jina mbadala la Pablo Escobar,"El Patron,", wateja wake umeongezeka kwa mara mbili.
MADAWA YA KULEVYA NA DINI:
Papa Francis alikuja Colombia kuunga mkono jitihada zake za kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilikuwa vinatokana na biashara ya madawa ya kulevya.
Serikali imefanya amani na kundi kubwa la waasi la FARC, kundi ambalo limejijenga na kufadhiliwa na biashara ya madawa ya kulevya.
Umoja wa Mataifa unaitambua Colombia kama mzalishaji mkuu duniani wa koka ambayo ni malighafi ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine.
Lakini mbali na kuwa mji unaohusishwa na makundi ya madawa ya kulevya nchini Colombia, Medellin pia ni wazi kuwa ni jiji la Wakatoliki wengi.
Mji huo wenye wakazi milioni mbili, inasemekana kuwa ndio wenye makanisa zaidi kuliko mji mwingine wowote katika nchi hiyo yenye watu takribani milioni 48.
Katika nyumba yake iliyopo katika Wilaya ya Pablo Escobar, Wberney Zabala ana shimoni ndogo (sehemu ya kufanya ibada)yenye picha ya bosi huyo wa zamani wa madawa ya kulevya iliyopambwa kwa picha zake na mishumaa.
"Hakuna kiongozi wa dini na hakuna mwanasiasa anayeweza kumzidi Pablo," alisema Zabala, mwenye umri wa miaka 45, askari aliyekuwa mlemavu na sasa ni kiongozi wa jamii.
"Kujenga makazi haya ilikuwa ni muujiza wake wa kwanza ... kadili makazi haya yanavyoendelea ndivyo hadithi yake itakavyokuwa."
CHANZO:
yahoo.com/news
Comments
Post a Comment