BILL GATES. Picha: Getty. |
Jumuiya ya kimataifa inaweza kuwa na kipaumbele juu ya suala la vita vya nyuklia, lakini viongozi wa ulimwengu wanaangalia upande mmoja, kuna tishio kubwa la Virusi vya magonjwa vilivyotengenezwa na binadamu
Hivyo ndivyo bilioniea Bill Gates alisema wakati wa Mkutano wa Usalama,Munich, nchini Ujerumani kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Washington Post la Marekani.
Gates aliwaambia viongozi wa ulimwengu kwamba ugaidi wa kibaiolojia(bioterrorism), uwe wa kawaida unaotokea au uliofanywa na watu, una uwezo wa kuua watu zaidi kuliko silaha za nyuklia.
"Janga hili la pili lina uwezekano mkubwa wa kuwa na asili kutoka kwenye skrini ya kompyuta"
Bilionea huyo tajiri zaidi ulimwenguni aliongeza kusema kuwa janga hili linaweza kuua mamilioni ya watu.
Pia Gates alisisitiza kuwa serikali za ulimwengu mzima zinapaswa kujiandaa na janga hilo kama wanavyojiandaa na vita.
CHANZO:
fortune.com
Comments
Post a Comment