DK.SUZAN KOLIMBA. Picha: The Citizen. |
Tanzania ni kati ya nchi saba ambazo zinashutumiwa kukiuka vikwazo vya silaha vilivyowekwa na umoja wa mataifa (UN) dhidi ya Korea ya kaskazini, kulingana na ripoti ya wataalamu wa ufuatiliaji wa vikwazo hivyo ,Ripoti hiyo ilitolewa Jumamosi.
Nchi nyingine ambazo zinahusishwa katika ripoti hiyo ni Angola, Kongo, Eritrea, Msumbiji, Namibia, Uganda na Syria.
Hata hivyo, Naibu waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa Dk.Suzan Kolimba amesema kuwa serikari haijui ripoti hiyo.
"Hatukupokea mawasiliano yoyote, kwa hiyo siwezi kutoa maoni ... tutaweza kutoa na maoni sahihi wakati tutakapokua tumeiona taarifa hiyo,"
Dk.Kolimba aliliambia gazeti la Citizen,Tanzania katika mahojiano ya simu.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Serikali ya Kim Jong Un iliendelea kukiuka vikwazo vikali ilivyowekewa juu ya bidhaa, silaha na vikwazo kwenye shughuli za usafirishaji kwa njia ya meli na fedha.
Ripoti hiyo ilitolewa kwa umma siku mbili kabla ya Marekani kupiga kura juu ya uamuzi mpya wa vikwazo.
Rasimu ya awali ya Marekani ingeweka vikwazo vikali zaidi kwa Korea ya Kaskazini ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku mauzo ya gesi na mafuta ya asili kwa nchi na kufungia mali zote za kigeni za serikali na kiongozi wake Jong-un.
Katika ripoti wataalam walisema pia wanachunguza ripoti kwamba kampuni ya Korea ya kaskazini inatengeneza na kuimarisha mifumo ya Tanzania ya mokombora ya kutokea ardhini(surface-to-air missile systems), kitu ambacho Dr. Kolimba alisema hakijui.
Linapokuja swala vikwazo vya kifedha, jopo hilo linasema Korea ya Kaskazini inaendelea kuepuka na kukiuka kwa njia kadhaa: Taasisi zake za kifedha nyingi huhifadhi wawakilishi wa ng'ambo ambao hufanya shughuli zinazowezesha mipango iliyozuiliwa.
Inadaiwa kuwa Korea ya Kaskazini imesafirisha nje makaa ya mawe, chuma na bidhaa nyingine kwa kiasi kikubwa cha thamani ya dola milioni 270 kwa China na nchi nyingine ikiwa ni pamoja na India, Malaysia na Sri Lanka katika kipindi cha miezi sita kinachokoma mapema Agosti kwa kukiuka vikwazo,
Wataalamu hao wa umoja wa mataifa wanadai .
Kati ya Desemba 2016 na Mei 2017, kwa mfano, Korea ya Kaskazini ilifirisha zaidi ya dola milioni 79 za chuma nchini China, Ripoti hiyo ilisema.
Na kati ya Oktoba 2016 na Mei 2017, ilitoa bidhaa za chuma na chuma kwa Misri, China, Ufaransa, India, Ireland na Mexico yenye thamani ya $ 305,713.
CHANZO:
thecitizen.co.tz
Comments
Post a Comment