Picha: PA. |
Ruud Van Nistelrooy anakumbukwa kama mmoja wa wafungaji bora kuwahi kucheza katika timu ya Manchester United ya Uingereza.
Lakini pamoja na kufunga mabao 95 katika klabu hiyo, aliishia kuuzwa kwa timu ya Real Madrid ya Hispania.
Ilikua inafahamika kwamba Van Nistelrooy alifika kikomo katika klabu hiyo kubwa ya Uingereza baada ya tabia zake zisizokubalika alizozionesha wakati wa fainali ya kombe la Carling mwaka 2016. Inasemekana kuwa mchezaji huyo alipishana kwa maneno na kocha wake, Alex Ferguson kwasababu hakupangwa hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba kwenye mechi hiyo dhidi ya Wigan Athletic.
Punde baada ya mtafaruku huo na kocha Alex Ferguson mchezaji huyo aliuzwa Real Madrid na kilichofuata ni historia.
RUUD VAN NISTELROOY WAKATI ALIPOKUA REAL MADRID. Picha: AFP/ Getty. |
Lakini miaka 11 baada ya Van Nistelrooy kuondoka klabuni Manchester United, sehemu ya kitabu cha mkuu wa zamani wa mawasiliano ya wafanyakazi wa klabu hiyo, Alastair Campbell, kinaonesha kwamba moja kati ya sababu za kuondoka kwa Van Nistelrooy inahusishwa na Cristiano Ronaldo.
Campbell ambaye alikua rafiki mkubwa wa kocha Alex Ferguson alisema kuwa Ferguson alimweleza kuhusu kuondoka kwa Van Nistelrooy na kwa namna gani ni vigumu kuwa meneja wa Van Nistelrooy.
"Tatizo lake la mwisho ni pale alipomwambia Cristiano Ronaldo kuwa amepata baba mwingine, yaani Carlos Queiros (msaifizi wa Ferguson) muda mfupi baada ya baba yake Ronaldo kufariki."
,aliandika Campbell.
"Carlos alimwambia aoneshe heshima lakini Van Nistelrooy akasema kuwa haheshimu mtu yeyote klabuni hapo...baadae akaomba msamaha...lakini Ronaldo hakumsamehe."
" Ferguson alimrudisha nyumbani Van Nistelrooy baada ya kusikia alichofanya wakati bado akiwa hana uwakika atamfanya nini"
, Campbell aliendelea kufafanua kwenye kitabu hicho.
Picha: PA. |
Ruud Van Nistelrooy alikwenda Real Madrid, na baadae Hamburg ya Ujerumani na kumalizia soka timu ya Malaga ya Hispania mwaka 2012'
CHANZO:
sportsbible.com
Comments
Post a Comment