YOUSSOUFA MOUKOKO. |
Baba wa mchezaji mwenye umri wa miaka 12 ambaye amefunga mara tatu katika mechi ya kimataifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 16 ya Ujerumani amewatoa wasiwasi watu juu ya umri wa kweli wa mwanawe.
Youssoufa Moukoko ambae ni mzaliwa wa Cameroon, , alifunga goli lake la kwanza dhidi ya Austria Jumatatu na goli la pili dhidi ya upande huo huo katika ushindi wa 2-1 Jumatano.
Pia amefunga mabao 13 katika michezo mitano kwa Borussia Dortmund chini ya miaka 17.
"Mara tu baada ya kuzaliwa, nilijisajili katika ubalozi wa Ujerumani huko Yaounde," alisema baba yake, Joseph.
"Tuna cheti cha kuzaliwa Kijerumani."
Kwa mujibu wa hati yake ya kuzaliwa rasmi, Moukoko alizaliwa tarehe 20 Novemba, 2004 nchini Cameroon.
Kulikuwa na maswali katika vyombo vya habari vya Ujerumani juu ya umri wa kweli wa kijana huyo, lakini Chama cha Soka cha Ujerumani (DFB) amesema makaratasi yake yote hayana matatizo.
"DFB tayari imekuwa na majadiliano mazuri na Borussia Dortmund katika ngazi mbalimbali," ilisema taarifa.
"Hakuna shaka juu ya usahihi wa umri wa mchezaji."
Chini ya sheria za DFB, Moukoko hawezi kuruhusiwa kucheza Bundesliga hadi akiwa na umri wa miaka 17.
CHANZO:
Comments
Post a Comment