Skip to main content

MWANAMUZIKI WA KENYA ,STELLA MWANGI AZIDI KUTAMBA HOLLYWOOD.

STELLA MWANGI.


Mwanamuziki wa Kenya, Stella Mwangi anaendelea kuwika katika tasnia ya filamu za Hollywood baada ya nyimbo yake nyingine kuchaguliwa kutumika katika filamu kubwa nchini Marekani.

  Filamu hiyo inayojulikana kama
"BAD MOMS CHRISTMAS" inatarajiwa kuzinduliwa mwezi Desemba mwaka huu (2017).

Tazama hapa kipande cha filamu "BAD MOMS CHRISTMAS" :




Nyimbo hiyo hiyo tayari ilishatumika katika msimu wa pili wa HBO TV Show inayoitwa "INSECURE"

STL ametumia akaunti yake ya Instagram kuwashawishi mashabiki zake kuingalia filamu hiyo pindi itakapotoka.

Filamu hiyo imesheheni waigizaji mashuhuri wa Hollywood kama Mila Kunis ,Kristen Bell , Kathryn Hahn , Susan Sarandon na kadharika.

Nyimbo ya mwanamuziki huyo wa kughani kutoka Kenya ambae anaendesha shughuli zake nchini Norway ,"SET IT OFF" sasa inakua ni mara ya pili ndani ya mwaka (2017) huu kutumika kwenye filamu kubwa za Hollywood.

Nyimbo yake nyingine ,"BAD GIRL" nayo ilitumika katika filamu nyingine ya Hollywood iliyotoka mwezi Julai mwaka huu , "ROUGH NIGHT"
Filamu hiyo ilikua na waigizaji wakubwa kama Scarlett Johansson , Kate McKinnon , Zoe Klavitz , Gillian Bell na Llaa Glazer.

CHANZO:
nairobinews.nation.co.ke

Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

UTATA WA FORM 34A FEKI KATIKA TOVUTI YA IEBC.

  Na BERNADINE MUTANU  Imepakiwa - Wednesday, August 16   2017 at  11:11 Kwa Mukhtasari VISA vya dosari kwenye uchaguzi uliokamilika vinazidi kuripotiwa nchini Kenya, wiki moja baada ya wananchi kupiga kura, na siku kadhaa baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutangaza mshindi wa urais. Huku IEBC ikikosolewa kwa kutangaza matokeo ya mwisho ya urais Ijumaa usiku kabla ya matokeo yote kuingia, imeibuka kuwa kituo kimoja Kaunti ya Mandera kilitumia karatasi ya kawaida kurekodi matokeo ya urais, badala ya kutumia Fomu 34 A. Matokeo hayo yaliwekwa katika tovuti ya IEBC, na kushangaza wananchi, huku madai ya wizi wa kura yakizidi kuchacha. 'Fomu’ hiyo isiyo ya kawaida iliwekwa katika mtandao wa IEBC kutoka Kituo cha Kuhesabia kura cha Bulla Dadacha 2, Wadi ya Elwak Kusini, Eneo Bunge la Mandera Kusini, Kaunti ya Mandera. Haina nambari ya mfuatano  (serial number)  kama fomu za kawaida za uchaguzi,...

MCHEZAJI WA ZAMANI WA UINGEREZA AMESEMA ALICHEZA NA WACHEZAJI WATATU MASHOGA KWENYE TIMU.

Carl Hoefkens (jezi no.2) alichezea West Bromwich Albion na Stoke City wakati wa enzi zake ligi kuu ya England. Beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza amesema alicheza pamoja na wachezaji wenzake wawili wa mashoga ndani ya timu, na mmoja alikua na jina kubwa. Carl Hoefkens, West Bromwich Albion na Stoke City siku za nyuma, anasema wachezaji hao walikua wazi na hawakujificha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingawa bado hawajulikani kwasababu ya maombi yao wenyewe ya kuomba kutotangazwa. Justin Fashanu, ambaye alijiua mwaka 1998, alikuwa mchezaji wa mwisho wa kazi nchini England kuja nje kama mashoga - mwaka 1990. Hoefkens alipokua (kushoto), alipokua anachezea Stock  City. Hoefkens aliyecheza Uingereza kwa miaka minne, akiondoka mwaka 2009, alidai kuwa mchezaji mwenzake mmoja wa timu alikua anaweza kuja kwenye uwanja wa mafunzo ya klabu na mpenzi wake wa kiume  lakini aliwaomba wenzake kutokuwaambia watu wangine wa nje ya timu. 'Nilicheza pamoja n...

KIONGOZI MKUU WA UPINZANI NCHINI ZIMBABWE, MORGAN TSVANGIRAI AMEFARIKI DUNIA.

Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika Kusini, afisa mkuu wa chama chake cha MDC amesema. Bw Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 65, aliyekuwa waziri mkuu, alilipotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na saratani ya koloni. "Amefariki jioni hii, familia yake imenitaarifu"  Makamu wa Rais wa MDC, Elias Mudzuri aliliambia shirika la habari la Uingereza, Reuters. Morgan Tsvangirai alizaliwa mnamo Machi 10, 1952 huko Gutu, Zimbabwe. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa mgodi, fundi, na mkulima. Alihudhuria Shule ya Msingi ya Guco ya St. Marks. Kisha alihamishiwa Shule ya Msingi ya Chikara Gutu. Kwa elimu yake ya sekondari, alihudhuria Shule ya High Gokomere. Alikuwa waziri mkuu katika serikali ya mseto ya Zimbabwe tangu 2009 hadi 2013. Katika kazi yake ya awali alionekana kuwa mfanyakazi mwenye bidii sana na alifanya kazi katika mgodi wa madini ya nickel( kwa zaidi ya muongo mmoja. Alipanda cheo haraka kutambuliwa na akain...

JINSI YA KUOMBA PASSPORT YA TANZANIA KWA NJIA YA INTERNET.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia i dara ya Uhamiaji  imezindua huduma ya ujazaji fomu za maombi ya hati ya kusafiria (Passport) kwa njia ya mtandao, ambapo mwombaji atalazimika kujaza fomu hizo na kuzichapisha kabla ya kuziwasilisha kwenye ofisi za uhamiaji. Idara hiyo pia imeeleza kuwa matumizi ya huduma hiyo yataenda sambamba na huduma inayotumiwa sasa ya fomu za maombi ya pasipoti mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo. Huduma hiyo itaanza kufanya kazi kuanzia Jumatatu tarehe  7/8/2017    na unaweza  kujaza fomu hizo  kwa kufungua tovuti hiyo ambayo ni  https://www.immigration.go.tz/ppt_application/ Utaratibu wa namna ya kujaza fomu hizo umeelekezwa katika fomu husika mtandaoni, na pia wateja wanaweza kupata ufafanuzi au maelezo zaidi kuhusu huduma hiyo kupitia anuani ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni   info@immigration.go.tz   au katika Ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyo karibu yako. CHANZO: http://dibute.com/muhimu-...

NAKUMATT IMEPATA TUZO YA MLIPAKODI BORA NCHINI RWANDA.

MENEJA WA NAKUMATT NCHINI RWANDA, ADAN RAMATA, AKIPOKEA TUZO YA MLIPA KODI BORA KUTOKA KWA MWENYEKITI WA SHIRIKISHO LA SEKTA BINAFSI LA RWANDA, BENJAMIN GASAMERA. KIGALI, Rwanda, Oktoba 16 Kampuni ya maduka ya kuuza bidhaa za rejareja ya Nakumatt imetangazwa kuwa walipa kodi bora na Mamlaka ya Mapato ya Rwanda. Nakumatt Rwanda ambayo inafanya kazi maduka ya rejareja 3 jijini Kigali, Rwanda ilitangazwa mlipakodi bora Ijumaa jioni katika tukio ambalo liliandaliwa na RRA ili kusherehekea walipa kodi katika nchi. Nakumatt Rwanda ilichukua tuzo bora ya walipa kodi ya 2016. Kampuni hiyo pia ilipokea tuzo bora ya mtumiaji wa umeme wa EBM (EBM). Akizungumza katika tukio hilo, Kamishna Mkuu wa RRA Richard Tusabe alithibitisha kwamba kiwango vya kulipa kodi nchini kimekuwa kwa kasi na kutokana na ushirikiano mzuri kutoka katika sekta kadhaa za uchumi ikiwa ni pamoja na sekta binafsi. Mkurugenzi huyo wa RRA alifafanua kuwa bodi ya kodi imeweza kufika lengo lake la kukusanya katika...

BAYERN MUNICH WANAJENGA VYUMBA VYA HOTELI NDANI YA UWANJA.

Huu ndio utakaokuwa muonekano wa vyumba hivyo kwa ndani. Picha: Mariot International. Kama sehemu ya mpango wa miaka mingi ya Bayern na  kampuni kubwa ya hoteli za Mariot na Courtyard, mashabiki hivi karibuni wataweza kupata fursa ya kukaa katika vyumba ambavyo vina dirisha linaloangalia uwanja wa Alianz Arena moja kwa moja. Vyumba hivyo vya kifahari vya kulala vitakuwa na kitanda cha kikubwa na seti ya televisheni - tu ikiwa umechoka na hat-trick za Robert Lewandowski. Pia kutakuwa na mahali pa moto ambayo ni maalumu kwa siku za mechi kwenye majira ya baridi. Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alisema: "Tunafurahia bidhaa mbili zinazoongoza kama hoteli Courtyard zinazomilikiwa na kampuni ya Marriott na FC Bayern kuingia katika ushirikiano huu wa muda mrefu kibiashara. "Tunapendezwa na bidhaa mbili zinazoongoza kama Courtyard na Marriott na FC Bayern kuingia katika ushirikiano wa muda mrefu," "Kutokana na kwamba Marri...

NAPE ASEMA KWAMBA TUNDU LISSU ALIMWAMBIA WANATAFUTWA, AHAME CCM.

MBUNGE WA MTAMA (CCM) AKICHEKA NA TUNDU LISSU MUDA MFUPI KABLA YA KUPIGWA RISASI. Imeandikwa na Edwin Mjwahuzi , Mwananchi; emjwahuzi@mwananchi.co.tz Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (kulia) akifurahia jambo na mbunge wa Mtama, Nape Nnauye walipokuwa wakitoka kuhudhuria kikao cha Bunge, mjini Dodoma jana mchana. By Edwin Mjwahuzi, Mwananchi; emjwahuzi@mwananchi.co.tz Dodoma. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ameeleza alichoambiwa na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana Alhamisi mchana wakati wakitoka bungeni huku wakicheka. Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe ni watuhumiwa, hama CCM mjomba.” Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya. Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini jana wakati Lissu...