Na BERNADINE MUTANU
Imepakiwa - Wednesday, August 16 2017 at 11:11
Kwa Mukhtasari
VISA vya dosari kwenye uchaguzi uliokamilika vinazidi kuripotiwa nchini Kenya, wiki moja baada ya wananchi kupiga kura, na siku kadhaa baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutangaza mshindi wa urais.
Huku IEBC ikikosolewa kwa kutangaza matokeo ya mwisho ya urais Ijumaa usiku kabla ya matokeo yote kuingia, imeibuka kuwa kituo kimoja Kaunti ya Mandera kilitumia karatasi ya kawaida kurekodi matokeo ya urais, badala ya kutumia Fomu 34 A.
Matokeo hayo yaliwekwa katika tovuti ya IEBC, na kushangaza wananchi, huku madai ya wizi wa kura yakizidi kuchacha.
'Fomu’ hiyo isiyo ya kawaida iliwekwa katika mtandao wa IEBC kutoka Kituo cha Kuhesabia kura cha Bulla Dadacha 2, Wadi ya Elwak Kusini, Eneo Bunge la Mandera Kusini, Kaunti ya Mandera.
Haina nambari ya mfuatano (serial number) kama fomu za kawaida za uchaguzi, haina majina ya maajenti waliosimamia uchaguzi, afisa wa IEBC aliyesimamia kituo hicho, idadi ya wapigakura na kura zilizokataliwa, au hata jina la kituo chenyewe kama zilivyo fomu zingine.
Rais Uhuru Kenyatta katika matokeo kutoka kituo hicho alikuwa na kura 323, Raila Odinga 40, Abduba Dida 18 na kura zilizoharibika zilikuwa nne.
Matokeo hayo hayajaonyesha walichopata wagombea wengine watano wa urais.
Comments
Post a Comment