KAMISHNA WA KAUNTI YA KIAMBU ALEX OLE NKOYO (kulia) AKIZINDUA PIKIPIKI 12 ZILIZOTOLEWA NA KWA MACHIFU NA MANAIBU WAO MAPEMA 2016. |
Japo umekuwa ukitekelezwa kwa siri, mpango huo unaojulikana kama Cell Thirty (C30), unalenga kuhakikisha watu wamejitokeza kwa wingi vituoni na maafisa wa utawala wa mikoa wameagizwa kuhakikisha umefaulu.
Chifu mmoja aliyeomba tusitaje jina lake ili asidhulumiwe alisema mikutano 15 ya siri iliandaliwa tangu Julai katika kaunti zote. Alieleza kwamba machifu wamekabidhiwa nakala za sajili ya wapigakura katika maeneo yao ili waweze kuwafuatilia kesho.
Katibu Mkuu wa wizara ya usalama wa ndani Dkt Karanja Kibicho aliongoza mkutano wa machifu wote 250 kutoka kaunti ya Nyeri. Mkutano huo ulifanyika Kiamuiru Gatitu Julai 23.
atibu Mkuu wa wizara ya usalama wa ndani Dkt Karanja Kibicho aliongoza mkutano wa machifu wote 250 kutoka kaunti ya Nyeri. Mkutano huo ulifanyika Kiamuiru Gatitu Julai 23“Tumeagizwa kuhakikisha kuwa kila mmoja amefikisha watu 30 wamefika kituoni kumpigia kura rais,” alifichua chifu huyo.
Katika mpango huo wazee wa mitaa, viongozi wa kidini, wasanii na wafanyabiashara wameshirikishwa kuhakikisha watu watajitokeza vituoni.
Machifu wamekuwa wakipatiwa pesa kutoka kwa maafisa wa serikali na wafanyabiashara watajika eneo hilo ili kufanikisha mpango huo.
Wanaongoza mpango huo tayari wamelipwa na kukagua sajili ya wapigakura na kuwafuatilia wote waliosajiliwa kujua waliko.
Watapokea malipo ya mwisho Jumatatu jioni na wameahidiwa zawadi nono wakitimiza malengo yao.
“Waliohusishwa katika mpango huo kama vile wazee wa mitaa walichaguliwa kwa sababu wanaelewa maeneo yao na kufahamu kila mtu wanakotoka,” alieleza chifu huyo.
Aliongeza kuwa wamepatiwa firimbi na vuvuzela ambazo watapuliza saa kumi alfajiri kesho kuwaamsha wakazi na kuwashinikiza kwenda kupiga kura.
Kila kituo cha kupiga kura kitakuwa na magari na pikipiki za kutumia kwenda kuwabeba wapigakura wagonjwa, wazee na walemavu.
“Tulifahamishwa kwamba kura ya urais itashindwa ikiwa wapigakura watajitokeza kwa wingi. Awali, walijaribu kutumia mpango wa Nyumba Kumi, vikundi vya kijamii lakini haukufaulu wakati huo.
Changamoto ya mpango huo ni kuwa wanasiasa wa eneo hilo wanajaribu kuuingilia wakitaka wanaoutekeleza kuwaagiza wapigakura kuwachagua.
Mpango huo ulitumiwa wakati wa usajili wa wapigakura mnamo Februari mwaka huu.
Kuna wapigakura zaidi ya 4,457,392 katika kaunti kumi za eneo la Mlima Kenya.
Kaunti hizo ni Nyeri, Murang’a, Kirinyaga, Nyandarua, Laikipia, Kiambu, Embu, Meru, Tharaka Nithi na Isiolo. Kuna jumla ya vituo 8858 vya kupigia kura katika kaunti hizo.
CHANZO:
Comments
Post a Comment