Skip to main content

ALICHOSEMA SHEIKH PONDA KUHUSU MIILI INAYOOKOTWA BAHARINI.

SHEIKH PONDA.


KUTOKA GAZETI LA NIPASHE ,22 Agosti 2017;

Akizungumza na Nipashe kwa simu jana, Sheikh Ponda ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania, alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakipaza sauti kuhusu uwapo wa mauaji ya raia kwenye mikoa ya kusini mwa Tanzania, lakini haijasikilizwa.


"Tunapongeza Nipashe kwa habari hii," alisema Sheikh Ponda kwa sababu "imefichua mambo mengi.",
"Haya tumeshayasema lakini hakuna aliyetusikiliza.
"Ni wakati mwafaka serikali ikatoa tamko kwa vile vyombo vya dola vimeonyesha kushindwa kueleza miili hiyo ni ya watu gani na inatoka wapi, (na kibaya) zaidi wanasema wanatambua miili mitatu iliyookotwa ambayo kwa sasa iko Muhimbili."


Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya, aliiambia Nipashe kwa njia ya simu juzi kuwa miili iliyookotwa ni mitatu na haikuwa kwenye viroba.


Sheikh Ponda alisema mauaji hayo ni makubwa na hayajawahi kutokea kwa serikali zilizopita kwa miili kusambaa baharini na wavuvi kuiopoa.
Alisema jambo hilo si la kawaida, lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa wala kutolewa taarifa ya kina na serikali kuhusu hali hiyo.

"Jumuiya inaona ni wakati mwafaka kwa serikali kutueleza kwa kuwa vyombo vya dola havijui au havitaki kutoa taarifa juu ya kile kinachoendelea hadi maiti kuokotwa zikiwa ndani ya viroba baharini," alisema.
Sheikh Ponda alisema kunapokuwa na masuala mazito kama hayo, kauli ya serikali inahitajika ili kujua ukweli na uhakika wa ulinzi kwa wananchi wake.
Wavuvi na wafanyabiashara katika masoko na minada ya samaki ya Kunduchi, Ununio na Feri jijini Dar es Salaam waliiambia Nipashe mwishoni mwa wiki kuwa wanaishi kwa hofu baada ya kuopolewa miili 15 ya watu baharini ikiwa imewekwa katika mifuko maalumu kama viroba, Bara na Zanzibar katika siku za karibuni.
Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika vilivyozungumza na Nipashe, miili hiyo iliokotwa kwa nyakati tofauti na wavuvi ambao waliwajulisha polisi, waliofika kuichukua.
Kuwapo kwa idadi kubwa ya miili inayoopolewa kutoka baharini au kukutwa fukweni ikiwa imefungwa kama mzigo kumefanya wavuvi na wafanyabiashara wa samaki kaskazini mwa wilaya ya Kinondoni kuingiwa na hofu pia.


Mwanaharakati huyo pia alirusha lawama kwa Bunge akidai kuwa chombo hicho cha kutunga sheria kimeshindwa kufanyia kazi barua yao ya Julai 14, mwaka huu, yenye kumbukumbu namba JTKT/BJMT/1/17 kuomba kuundwa kwa kamati huru ya Bunge, kufanya uchunguzi wa mauaji ya raia kwenye maeneo ya ukanda wa kusini.

"Tuliona kabisa haifai kutegemea taarifa za upande mmoja, yaani Jeshi la Polisi pekee, bali tuwe na chombo huru kitakachotokana na chombo cha uwakilishi wa wananchi, wakienda kuchunguza wataleta taarifa huru na kujua ukweli wa mambo," alisema na kueleza zaidi:
"Cha kusikitisha Spika hakujibu barua yetu kabisa.

"Tafsiri ya haraka ni kuwa uwakilishi wa wananchi kwenye chombo hicho uko wapi? Wito wetu uko palepale, jambo hili siyo la kuacha lipite bure, tunataka kuona hatua zikichukuliwa."
Nipashe ilimtafuta Spika Job Ndugai kuhusu lawana hizo za Sheikh Ponda dhidi ya Bunge, lakini simu yake ilikuwa haipatikani na hakujibu ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) aliotumiwa.


KUOPOLEWA MIILI

Nipashe pia ilimtafuta Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, ambaye alikiri kuopolewa kwa miili kwenye fukwe za Bahari ya Hindi imefungwa kwenye viroba.
"Zipo maiti zimeopolewa na wavuvi katika Pwani ya Dar es Salaam, zikiwa ndani ya mifuko zimeshonewa ndani," DCI Boaz alithibitisha.
Alipoulizwa idadi na maeneo zinakotoka na zinakohifadhiwa, alisema: "Hilo waulize makamanda wa polisi wa mikoa ya kipolisi, siwezi kuwa na takwimu hizo."
Alisema zaidi: "Pia kuhusu zinatoka wapi ni mapema sana kujua kwa kuwa zimebebwa na mawimbi ya bahari hadi kuokotwa maeneo husika.
"Bahari ni pana sana na maiti hizo zinasombwa na mawimbi, hatujui zinatoka wapi, ila waulize maRPC (makanda wa polisi) wa mikoa husika."


Wavuvi waliozungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki walisema uwapo wa idadi kubwa ya miili hiyo umesababisha baadhi yao kunyamaza wanapoona miili zaidi ikielea baharini.
“Polisi tunawajulisha, wanakuja, wanabeba maiti lakini hakuna siku wametueleza ni za kina nani," alisema mvuvi mmoja wa Kunduchi aliyezungumza na Nipashe kwa sharti la kutotajwa jina gazetini akihofia usalama wake.
"Wavuvi tunafahamiana na ikitokea mwenzetu amekufa au chombo kimezama majini tunafahamu.
"Lakini tangu Agosti mwanzoni tunaokota miili ikiwa imeandaliwa (imefungwa) kabisa na siyo ya wenzetu.”

Wavuvi hao walisema wamepokea taarifa kutoka kwa wenzao wa eneo la Kizimkazi, Zanzibar, kwamba huko nako pia zimeokotwa maiti tano.

Mvuvi mmoja wa Kunduchi alisema siku mbili zilizopita ziliokotwa maiti tano katika eneo la Bongoyo na nne nyuma ya kisiwa cha Mbudya, jijini Dar es Salaam.
Alisema kati ya maiti tisa hizo, moja ilikuwa ya mwanamke na kwamba zilikuwa zimefungwa kamba miguuni, kichwani na tumboni.
"Zote zilikuwa zimeharibika na sura hazitambuliki," alisema na kueleza kuwa zilichukuliwa na polisi baada ya kutaarifiwa.

Alisema polisi waliochukua miili hiyo ni wa mkoa wa Kinondoni kutoka vituo vya Kawe ambayo ni wilaya ya kipolisi na Wazo Hill.
"Hawajawahi kusema mtu huyo alifia wapi na chanzo cha kifo, (hivyo) wengi tuna wasiwasi tu," alisema mvuvi mwingine ambaye pia aliomba jina lake lihifadhiwe.
“Ukiangalia umri ni miaka 25 hadi 50.
"Jamaa zetu wa Feli waliokota maiti sita wiki mbili zilizopita (na) kati yake mbili zimefungwa pamoja na katika hizo moja ni mwanamke.
"Tulichozoea wavuvi ni kuokota maiti za wavuvi wenzetu ambaye alizama au kupotea, na zinakuwa na nguo zake za kawaida lakini hizi ni za kuandaliwa.”
Nipashe pia iliwatafuta viongozi wa serikali ya mitaa kwenye maeneo husika, ambao walisema wamelisikia suala hilo kutoka kwa wavuvi lakini waulizwe polisi.

CHANZO:
http://m.ippmedia.com/sw/habari/sheikh-ponda-afunguka-maiti-15-kwenye-viroba

Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

WASTANI WA ADA ZA VYUO VIKUU BORA ZAIDI DUNIANI.

            Elimu ya juu ya kupokea nje ya nchi (Nchi zilzo endelea) daima imekuwa kiwango cha kutambuliwa sana, na wanafunzi kutoka duniani kote siku zote wana ndoto kuhusu hilo.             Tovuti ya Bright Side imeamua kujua gharama za sasa za kujifunza * kwa wanafunzi wa kimataifa katika vyuo vikuu vya juu vya dunia, na tungependa kushiriki habari hii na wewe. * Wastani wa kila mwaka ada ya mafunzo ya shahada ya kwanza ; MAREKANI; Kwa maelezo zaidi kuhusiana na chuo hiki bonyeza hapa: http://www.harvard.edu/ Kwa maelezo zaidi kuhusiana na chuo hiki bonyeza hapa:  http://web.mit.edu/ UINGEREZA;     Kwa maelezo zaidi kuhusiana na chuo hiki bonyeza hapa; http://www.cam.ac.uk/     Kwa maelezo zaidi kuhusiana na chuo hiki bonyeza hapa: http://www.ox.ac.uk/ USWISI (SWITZERLAND ):     Kwa maelezo zaidi kuhusiana na chuo hiki bonyeza hapa:...

ORODHA YA NCHI ZA KWANZA NA ZA MWISHO KWA AMANI DUNIANI.

Marekani:  Ripoti ya Taasisi ya Uchumi na Amani imepata mataifa kumi tu ulimwenguni ambayo hayapo katika vita na migogoro kabisa. Kwa mujibu wa Ripoti ya Kimataifa ya Amani 2016, Botswana, Chile, Costa Rica, Japan, Mauritius, Panama, Qatar, Uswisi, Uruguay na Vietnam ndio nchi pekee ambazo hazipo kwenye vita wala migogoro yeyote ile ya kuhatarisha amani.. Iceland inaongoza orodha ya nchi zinazoongoza kwa amani ulimwenguni, ikifuatiwa na Denmark, Austria, New Zealand, Ureno, Jamhuri ya Czech, Uswisi, Canada, Japan na Slovenia - wakati Marekani ikiwa kwenye nafasi ya 103. Palestina imepanda kutoka nafasi ya 163 mpaka nafasi ya 148. Syria iliyoharibiwa na vita imewekwa chini ya orodha, chini kuliko Sudan Kusini, Iraq, Afghanistan, Somalia, Yemen, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ukraine, Sudan na Libya. "Ripoti inalinganisha amani duniani kwa kutumia mandhari tatu pana: hali ya utulivu na usalama katika jamii; kiwango cha mgogoro wa ndani au wa kimataifa; na kiwango cha kije...

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA GAMBIA AMTAKA RAIS WA TOGO KUACHIA MADARAKA KWA HIARI.

RAIS WA TOGO, FAURE GNASSINGBE. BANJUL, Oktoba 23 (Reuters) "Rais wa Togo Faure Gnassingbe anapaswa kujiuzulu mara moja na Umoja wa Afrika na kanda ya kikanda ya Afrika Magharibi ECOWAS inapaswa kumshawishi kushuka ikiwa hawaja fanya hivyo",  Waziri wa Mambo ya Nje wa Gambia Ousainou Darboe amesema. Maoni ya Darboe ni ishara ya mwanzo kwamba yuko dhidi ya Gnassingbe ambaye alinyakua madaraka kwa nguvu mwaka 2005 baada ya kifo cha baba yake ambaye alikuwa ametawala tangu mwaka 1967. Togo ni inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa ambao takribani watu 10 wameuawa katika maandamano tangu Agosti. "Nadhani Umoja wa Afrika na ECOWAS inapaswa kushiriki na kumshawishi rais wa Togo kung'ooka ," Darboe aliiambia Shirika la habari la Uingereza (Reuters) mwishoni mwa wiki hii, akiongezea kuwa nchi nyingine zinahitaji kushiriki. "Wakati serikali ya Togo inakiuka kanuni zinazokubalika sidhani kama suala hili linapaswa kuchukuliwa kama ni mambo ya ndani ya nd...

SABABU YA ZIPU NYINGI KUWA NA HERUFI "YKK".

Ikiwa umewahi kuchunguza kwa ukaribu zipu kwenye nguo zako nyingi, utakua tayari umeona herufi zinazosomeka "YKK," katika herufi kubwa, kwa mengi yao.Herufi hizi zipo kwenye kila kitu kutoka kwenye nguo za jeans, makoti hata kwenye mabegi. Herufi hizo zinasimama kwa niaba ya "Yoshida Kogyo Kabushikikaisha" ambayo, kutoka kwenye lugha ya Kijapani, inaelezea  "Yoshida Company Limited" yaani "Kampuni ya Yoshida"  Kampuni hii ni ya mtengenezaji wa zipu aitwaye Tadao Yoshida, ambaye aliianzisha mwaka wa 1934. Kwa wastani, kampuni hiyo inatengeneza nusu ya zipu duniani, ambayo ni zaidi ya zipu bilioni 7 kila mwaka. Kwa uhalisia Yoshida hakua mvumbuzi wa zipu duniani, zipu zilivumbuliwa na Mmarekani, Whitcomb L. Judson, miaka ya 1890.  Kampuni yake sasa ipo,  na inabuni na kutengeneza zipu za kisasa ikijulikana kama Talon, Inc. Bidhaa za kampuni hiyo hutumiwa makampuni kama Brooks Brothers na Uniqlo. Lakini YKK ina sifa isiyofananishik...

UGANDA IMEWAFUKUZA WATAALAM WA KIJESHI KUTOKA KOREA YA KASKAZINI.

Uganda imefukuza wataalamu wa kijeshi wa Korea Kaskazini na wawakilishi wa makampuni ya Kaskazini ya Korea, ikiwa ni pamoja na mfanyabiashara wake mkubwa wa silaha za juu kutokana na mataifa ya Kiafrika kukabiliwa na shinikizo la kuzingatia vikwazo vya Umoja wa Mataifa(UN) juu ya mpango wa silaha za nyuklia wa Pyongyang. "Raia wa Korea ya Kaskazini waliobaki katika taifa hilo la Afrika Mashariki ni wanadiplomasia na watu binafsi tu ", Okello Oryem, naibu waziri wa mambo ya kigeni, aliiambia The Associated Press. "Tunafuatana kabisa," alisema Oryem, akiongezea kwamba Uganda ina uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia na Korea Kaskazini. Uganda hasa ilidai kuondoka kwa watu wanaowakilisha Shirika la Biashara la Maendeleo ya Madini ya Korea. Ni mkataba wa msingi wa Korea Kaskazini na chini ya vikwazo vya U.N. na U.S. Uhamisho huo unaashiria mabadiliko ya sera kwa serikali ya Uganda, ambayo hapo awali ilikuwa na mahusiano ya mazuri na Pyongyang. Korea ya Kaska...

PAPA FRANCIS ASHINDANISHWA NA PABLO ESCOBAR KWA KUHESHIMIWA NCHINI COLOMBIA.

MedellĂ­n (Colombia) (AFP):  Katika saluni yake ya nywele, Yamile Zapata anatumia faida ya ziara ya Papa Francis ili kuuza pete za funguo zenye picha ya kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani. Lakini anadai sio ambapo pesa halisi iko kwenye mji wa Medellin nchini Colombia. Zawadi nyingi anazouza katika mji huu wa Colombia hubeba uso wa "mtakatifu" na shujaa wake mwenyewe: Pablo Escobar. Wakati Francis alikuwa akihudumia na kufundisha kama kuhani wa Yesuit katika miaka ya 1980, Escobar alikuwa akiua mamia ya watu na kufanya biashara ya madawa ya kulevya ya mabilioni ya dola za kimarekani. "Kila mtu anataka picha za papa sasa, lakini picha za Pablo zinauzika vizuri zaidi," , alisema Zapata, mwenye umri wa miaka 34, wakati ambao jiji hilo limeandaliwa kwa ajili ya mkutano wa Papa Francis wa wazi siku ya Jumamosi. PETE ZA FUNGUO ZENYE PICHA ZA PAPA FRANCIS NA PABLO ESCOBAR ZIKIWA ZINAUZWA KWENYE MITAA YA JIJI LA MEDELIN, COLOMBIA. Francis alitoa mane...

MCHEZAJI WA ZAMANI WA UINGEREZA AMESEMA ALICHEZA NA WACHEZAJI WATATU MASHOGA KWENYE TIMU.

Carl Hoefkens (jezi no.2) alichezea West Bromwich Albion na Stoke City wakati wa enzi zake ligi kuu ya England. Beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza amesema alicheza pamoja na wachezaji wenzake wawili wa mashoga ndani ya timu, na mmoja alikua na jina kubwa. Carl Hoefkens, West Bromwich Albion na Stoke City siku za nyuma, anasema wachezaji hao walikua wazi na hawakujificha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingawa bado hawajulikani kwasababu ya maombi yao wenyewe ya kuomba kutotangazwa. Justin Fashanu, ambaye alijiua mwaka 1998, alikuwa mchezaji wa mwisho wa kazi nchini England kuja nje kama mashoga - mwaka 1990. Hoefkens alipokua (kushoto), alipokua anachezea Stock  City. Hoefkens aliyecheza Uingereza kwa miaka minne, akiondoka mwaka 2009, alidai kuwa mchezaji mwenzake mmoja wa timu alikua anaweza kuja kwenye uwanja wa mafunzo ya klabu na mpenzi wake wa kiume  lakini aliwaomba wenzake kutokuwaambia watu wangine wa nje ya timu. 'Nilicheza pamoja n...