Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia idara ya Uhamiaji imezindua huduma ya ujazaji fomu za maombi ya hati ya kusafiria (Passport) kwa njia ya mtandao, ambapo mwombaji atalazimika kujaza fomu hizo na kuzichapisha kabla ya kuziwasilisha kwenye ofisi za uhamiaji.
Idara hiyo pia imeeleza kuwa matumizi ya huduma hiyo yataenda sambamba na huduma inayotumiwa sasa ya fomu za maombi ya pasipoti mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo.
Huduma hiyo itaanza kufanya kazi kuanzia Jumatatu tarehe 7/8/2017 na unaweza kujaza fomu hizo kwa kufungua tovuti hiyo ambayo ni https://www.immigration.go.tz/ppt_application/
Utaratibu wa namna ya kujaza fomu hizo umeelekezwa katika fomu husika mtandaoni, na pia wateja wanaweza kupata ufafanuzi au maelezo zaidi kuhusu huduma hiyo kupitia anuani ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni info@immigration.go.tz au katika Ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyo karibu yako.
CHANZO:
Comments
Post a Comment