Skip to main content

NAIROBI NI JIJI NAMBA 84 BORA DUNIANI KUWEKEZA,KUFANYA BIASHARA NA KUFANYA KAZI.





Na BERNARDINE MUTANU (TAIFA LEO /KENYA.
Imepakiwa - Monday, August 21   2017 at  15:54
Kwa Mukhtasari
JIJI la Nairobi limeorodheshwa katika orodha ya majiji 100 bora zaidi kwa kuanizisha biashara na kufanya kazi ulimwenguni.
Singapore, ndio mji bora zaidi katika kuanzisha biashara na kufanya kazi. Nchi hiyo pia iliorodheshwa bora kwa afya na usalama, na kufuatwa na Finland.
Ripoti hii ni kwa mujibu wa Nestpick. Shirika hilo lilitumia vigezo vitano kuorodhesha miji hiyo, ambavyo ni mandhari ya uanzishaji na ufanyibiashara, mishahara katika miji hiyo, usalama wa kijamii na marupurupu, gharama ya maisha, na ubora wa maisha.Kati ya miji yote iliyofanyiwa utafiti, Nairobi ilikuwa nambari 84. Miji ya kwanza 10 ni San Francisco, Berlin, Stockholm, Tel Aviv, Zurich, Seoul, Hamburg, na Toront.          Miji mingine iliyoorodheshwa barani Afrika ni Johannesburg (71), Cairo (80) na Tunis (83). Lagos imo katika  nafasi ya 85.
Watu wengi wanaweza kumudu gharama Nairobi lakini kwa kuzingatia kigezo cha mishahara, na usawa wa kijinsia, ilipata maki za chini ikilinganshwa na miji mingine iliyotafitiwa.

Watu wengi wanaweza kumudu gharama Nairobi lakini kwa kuzingatia kigezo cha mishahara, na usawa wa kijinsia, ilipata maki za chini ikilinganshwa na miji mingine iliyotafitiwa.

CHANZO:

Comments