KUTOKA SHIRIKA LA HABARI LA UINGEREZA;
DAR ES SALAAM (Reuters)
Kampuni ya Symbion inataka kulipwa dola milioni 561 za kimarekani na Shirika la usambazaji umeme la Tanzania (TANESCO) kupitia usuluhisho wa kimataifa kutokana na TANESCO kuvunja mkataba baina yao, kampuni hiyo ya Marekani imesema siku ya Jumanne.
Symbion inamiliki kituo cha kuzalisha nishati ya umeme wa megawati 120 katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam na ni moja kati ya wazalishaji wa wachache wa kujitegemea ambao huuza nishati kwa TANESCO.
Tanzania ina hifadhi ya gesi asilia ya tani milioni 57 lakini inakabiliwa na uhaba wa nishati ya umeme kwa muda mrefu kutokana na kutegemea mabwawa ya maji (hydro-power dams) katika ukanda unaoweza kukabiliwa na ukame, hivyo kulazimisha matumizi yake ya kununua nishati hiyo kutoka kwa makampuni binafsi.
Msemaji wa Symbion, Julie Foster, amesema wameishitaki TANESCO Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (International Chamber of Commerce's International Court of Arbitration) huko Paris Machi 13, wakisema TANESCO wameshindwa kuheshimu makubaliano ya miaka 15.
Foster alisema Symbion iliomba (arbitration) usuluhishi kwa sababu ilikosa kingine cha kufanya baada ya kushindwa kutatua mgogoro kwa njia ya kirafiki kwa zaidi ya mwaka mzima.
TANESCO ilikataa kutoa maoni, ikisema kuwa suala lilikuwa chini ya kesi za kisheria.
Rais wa Tanzania John Magufuli, aitwaye "Bulldozer" kwa ajili ya miradi yake ya miundombinu na mtindo wa uongozi mkali, alizindua mageuzi yake baada ya kuchaguliwa mwaka 2015, akiahidi kuimarisha uchumi uliopotea kwa urasimu na rushwa.
Lakini baadhi ya wawekezaji wa kigeni walisema wanaweza kusitisha shughuli zao au mipango ya upanuzi kwa sababu ya vigezo vigumu, ikiwa ni pamoja na bili za kodi za juu, kama sehemu ya raisi ya kubadilisha uchumi.
"Hata hivyo, wasiwasi huo ni kwamba mawazo ya muda mfupi, na sera zinazofuata, zinawafanya wawekezaji kuona kama serikali ya Magufuli haina urafiki wa kutosha na biashara," Ahmed Salim, Makamu wa Rais wa ushauri Teneo Intelligence, alisema katika taarifa kwa wateja Machi 6 (Kuhaririwa na Aaron Maasho / Ruth Pitchford)
Viwango vyetu: Thomson Reuters
CHANZO:
http://www.reuters.com/article/tanzania-power-symbion-idUSL2N1GY1T8
Comments
Post a Comment