Wakati filamu ya Hollywood iliyofahamika kama "Ghosts can't do it" ikiingia sokoni mwaka 1989 na kutokufanya vizuri kimapato, kwa upande mwingine ilikua na faida kwa mfanyabiashara maarufu wa marekani na Raisi wa sasa wa nchi hiyo Donald Trump katika tasnia ya maigizo.
Filamu hiyo ndiyo ilitoa fulsa ya kwanza kwa Donald Trump kupata kipande kidogo cha kuigiza kwenye filamu (cameo), kipande ambacho mchambuzi mashuhuri wa filamu wa kipindi hicho Bwana Roger Ebert alikiita ni kapande kinachofurahisha moyo.
Tazama kipande cha Video cha filamu ya kwanza ya Donald Trump kuigiza, "Ghosts can't do it" ;
Mwaka 1992,ulikua mwaka mzuri zaidi kwa Donald Trump wakati alipopata tena nafasi ya kuigiza katika filamu maarufu na iliyopata mafanikio makubwa kipindi hicho iliyojulikana kama "Home Alone 2". Katika filamu hiyo Donald Trump alionekana akimwelekeza mtoto Macaulay Culkin aliye igiza kama Kevin McAllister sehemu ya kupumzika wageni katika hoteli ya kifahari jijini New York. Ni wapenzi wachache sana wa filamu hiyo waliokua wanajua kwamba kwenye maisha halisi nje ya filamu, Hoteli hiyo ya kifahari ilikua ni mali ya Donald Trump aliyoinunua mwaka 1988.
Tazama kipande hicho cha filamu ya "Home alone 2" ;
Tangu kipindi hicho Donald Trump ambae sasa ni Raisi wa 45 wa Marekani alipata nafasi 12 za kuigiza katika filamu na runinga pamoja na tangazo la biashara maarufu la mwaka 1985 la "Pizza Hut"
Tazama hapa video ya vipande vya filamu na runinga vilivyowahi kuigizwa na Donald Trump ;
CHANZO:
http://www.washingtonexaminer.com/never-forget-donald-trumps-cameo-in-home-alone-2/article/2610290
Comments
Post a Comment