WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KOREA YA KASKAZINI,RI YONG-HO. |
Wanadiplomasia wa Korea ya Kaskazini wamewaomba wanasiasa wa Marekani kuwasaidia kunuelewa Donald Trump.
Habari mpya zilizoripitiwa na gazeti la Washington post zinasema kwamba wanadiplomasia wa Korea ya Kaskazini wanapata tabu kumuelewa Rais huyo mpya wa Marekani wakati wa kuongezeka kwa mvutano kati ya Washington na Pyongyang.
Hofu kuhusu kushindwa kutabiri maamuzi ya Trump imelazimisha wanadiplomasia hao wa Korea ya Kaskazini kufanya mazungumzo ya siri na wenzao wa Marekani, Kwa mujibu wa gazeti la Washington post.
"Kipaumbele chetu cha kwanza ni Trump, maana hatumuelewi kabisa"
Mmoja wao aliwaambia wanadiplomasia wa Marekani.
Pamoja na mazungumzo, hakuna dalili kwamba mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini yatafikiwa karibuni, ripoti hiyo ilisema.
Maneno hayo kutoka kwa maofisa wa Korea ya Kaskazini yakuja baada ya Rais Trump kuapa kuiangamiza nchi hiyo.
Rais Trump aliongeza kwa kudai kuwa rais Kim Jong Un amekua akifanya ukorofi na hivyo Marekani tayari imejiandaa kwa vita.
CHANZO:
thesun.co.uk
Comments
Post a Comment