Skip to main content

SABABU ZA MOURINHO KUSHIKWA NA HASIRA UWANJANI BAADA YA KUIFUNGA BASEL.

JOSE MOURINHO. (PA Wire)

Manchester United imeanza kwa kushinda kwenye Ligi ya Mabingwa kwa kumpiga kwa urahisi bingwa wa Uswisi Basel.

Lakini, licha ya mabao matatu ya United, Jose Mourinho alikasirika wakati wote akiwalaumu wachezaji wake wa kujiachia sana baada ya kupata magoli mawili.

Marouane Fellaini alifunga goli la kwanza katika nusu ya kwanza baada ya kupiga kichwa klosi ya Ashley Young, na Romelu Lukaku kufunga goli la pili mwanzo wa nusu ya pili ya mchezo.

Ni baada ya hapo ndipo Mourinho alionekana kutotulia uwanjani huku akitoa maelekezo mara kwa mara.

Kulikuwa na pasi nyingi zilizokuwa zinapotea hovyo kitu kilichofanya Mourinho aonekane kutokufurahishwa na wachezaji wake.

Akizungumza na BT Sport baada ya mchezo alisema: "Tulicheza vizuri mpaka 2-0. Baada ya hapo tuliisahau kucheza, tuliisahau kuimba, tuliacha kucheza kwa tahadhari, tuliacha kufanya maamuzi sahihi uwanjani, Tunaweza kujiweka katika matatizo lakini hakuweza kufunga. "

"Maamuzi mabaya, Soka la PlayStation, unapoacha kucheza kama timu na kuacha kucheza kwa uzito mimi sipendia ..."

"Labda wachezaji waliona mchezo huo ulikuwa chini ya udhibiti na 2-0 lakini soka ni soka na unapaswa kuwaheshimu wapinzani."

United wanongoza kundi A kwa tofauti ya magoli na Mourinho aliulizwa kama alichukizwa na kukosa magoli mengi zaidi.

Alijibu:
"Sidhani kama tofauti ya magoli itakwenda kuchukua nafasi yoyote.Hizi pointi tatu ni jambo muhimu zaidi, nilihisi tu baada ya 2-0 maamuzi yetu uwanjani yalikua katika mwelekeo usiofaa kabisa.
Tulipoteza nafasi, tulipoteza muundo wetu na tukapoteza mipira mingi sana kirahisi rahisi.. Nadhani wachezaji walijiachia sana na sikupenda. "

"Lakini kwa ujumla ya uchezaji ulikua imara na pointi tatu ni muhimu kwetu."


CHANZO:
manchestereveningnews.co.uk

Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

MCHEZAJI WA ZAMANI WA UINGEREZA AMESEMA ALICHEZA NA WACHEZAJI WATATU MASHOGA KWENYE TIMU.

Carl Hoefkens (jezi no.2) alichezea West Bromwich Albion na Stoke City wakati wa enzi zake ligi kuu ya England. Beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza amesema alicheza pamoja na wachezaji wenzake wawili wa mashoga ndani ya timu, na mmoja alikua na jina kubwa. Carl Hoefkens, West Bromwich Albion na Stoke City siku za nyuma, anasema wachezaji hao walikua wazi na hawakujificha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingawa bado hawajulikani kwasababu ya maombi yao wenyewe ya kuomba kutotangazwa. Justin Fashanu, ambaye alijiua mwaka 1998, alikuwa mchezaji wa mwisho wa kazi nchini England kuja nje kama mashoga - mwaka 1990. Hoefkens alipokua (kushoto), alipokua anachezea Stock  City. Hoefkens aliyecheza Uingereza kwa miaka minne, akiondoka mwaka 2009, alidai kuwa mchezaji mwenzake mmoja wa timu alikua anaweza kuja kwenye uwanja wa mafunzo ya klabu na mpenzi wake wa kiume  lakini aliwaomba wenzake kutokuwaambia watu wangine wa nje ya timu. 'Nilicheza pamoja n...

ORODHA YA NCHI 80 AMBAZO MTANZANIA ANARUHUSIWA KUINGIA BILA VIZA.

         Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza . Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza za kusafiria kama ilivyokuwa nchi za afrika Mashariki. Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni nchi ngapi ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza (viza on arrival). "Zipo nchi 16 kwa Afrika ambazo watanzania wanaweza kuzitembelea bila ya kuwa na viza na duniani zipo 67" alisema Masauni. Aidha Massauni amezitaja nchi hizo kuwa ni Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea­Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo. Pamoja na hayo Masauni amesema...

WALICHOJIBU CHENGE ,NGELEJA NA DK.KAFUMU BAADA YA RIPOTI YA PILI YA RAISI.

              VIGOGO waliotajwa katika ripoti ya pili ya kuchunguza makontena yenye mchanga wa madini (makinikia)  kuisababishia Serikali hasara ya matrilioni ya fedha kupitia sekta ya madini, walipokuwa wakihudumu katika nyadhifa zao serikalini wamevunja ukimya. Vigogo hao wamezungumzia ripoti hiyo ya pili iliyowasilishwa kwa Rais Dk. John Magufuli Ikulu Dar es Salaam jana, ambapo kamati husika ilichunguza hasara ambayo nchi imepata tangu 1998 usafirishaji wa mchanga wa dhahabu nje ya nchi ulipoanza. Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM), alipoulizwa maoni yake juu ya kutajwa na kamati hiyo, alisema hataki kuzungumza chochote juu ya ripoti hiyo, huku Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), akisema sheria ya madini ya 2010 ingefuatwa, nchi isingekuwa hapa ilipo. Kwa upande wake Kamishna wa Madini wa zamani, Dk. Dalaly Kafumu, alisema kwa sasa  hawezi kuzungumza jambo lolote kwa kuwa ni yeye ni mmoja wa watuhumiwa waliotaj...

KIONGOZI MKUU WA UPINZANI NCHINI ZIMBABWE, MORGAN TSVANGIRAI AMEFARIKI DUNIA.

Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika Kusini, afisa mkuu wa chama chake cha MDC amesema. Bw Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 65, aliyekuwa waziri mkuu, alilipotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na saratani ya koloni. "Amefariki jioni hii, familia yake imenitaarifu"  Makamu wa Rais wa MDC, Elias Mudzuri aliliambia shirika la habari la Uingereza, Reuters. Morgan Tsvangirai alizaliwa mnamo Machi 10, 1952 huko Gutu, Zimbabwe. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa mgodi, fundi, na mkulima. Alihudhuria Shule ya Msingi ya Guco ya St. Marks. Kisha alihamishiwa Shule ya Msingi ya Chikara Gutu. Kwa elimu yake ya sekondari, alihudhuria Shule ya High Gokomere. Alikuwa waziri mkuu katika serikali ya mseto ya Zimbabwe tangu 2009 hadi 2013. Katika kazi yake ya awali alionekana kuwa mfanyakazi mwenye bidii sana na alifanya kazi katika mgodi wa madini ya nickel( kwa zaidi ya muongo mmoja. Alipanda cheo haraka kutambuliwa na akain...

MADAI YA CUBA KWAMBA WAZIRI MKUU WA CANADA NI MTOTO WA FIDEL CASTRO.

Pichani ni waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau (kushoto), na Rais wa zamani wa Cuba, Hayati Fidel Castro (kulia). Maelezo yaliyoandikwa na mtoto wa kwanza wa rais wa zamani wa Cuba , Fidel Castro, kabla ya kujiua yamelishtua taifa la Cuba wiki hii. Maelezo hayo yaliyoandikwa na mtoto huyo mkubwa wa mwanamapinduzi na rais wa zamani wa nchi hiyo yalikuwa ya kushangaza baada ya  kuwa na madai ya kuwa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ni mtoto wa nje wa baba yake marehemu Fidel Castro. Maelezo hayo yaliyoandikwa kwa mkono na mtoto huyo wa Fidel Castro aliyejiua siku chache zilizopita kwa msongo wa mawazo, Fidel Castro Diaz-Balart, aliyekuwa na umri wa miaka 68, yalionekana kuthibitisha uvumi wa muda mrefu nchini Cuba kwamba Fidel Castro ni baba wa damu wa waziri mkuu wa sasa wa Canada, Justin Trudeau ikiwa ni matokeo ya uhusiano wa siri wa kimapenzi na mke wa mwanasiasa maarufu wa Canada, Pierre Trudeau, Margaret Trudeau mwaka 1970. Kifo cha mwanasayansi wa ...

KASHFA YA MAPENZI KATI MH.MBOWE NA WEMA SEPETU.

MH.FREEMAN MBOWE AKIWA NA WEMA SEPETU. Siku chache baada ya ile skendo ya ngono iliyosababisha wakili na mshauri wa Chama cha ACT -Wazalendo , Bwana Albert Msando kujiuzulu kwenye nyadhifa yake ya chama ,yameibuka mangine kwenye chama kikuu cha upinzani Tanzania ,CHADEMA ,baada ya kusambaa kwa kipande cha sauti kinachodaiwa kua ni mazungumzo kati ya mwenyekiti wa chama hicho na mbunge wa Hai Mh.Freeman Mbowe na Miss Tanzania 2006 ,mrembo Wema Isack Sepetu. SIKILIZA HIVI VIPANDE VYA SAUTI: Bonyeza hapa chini kusikiliza maongezi hayo yanayodaiwa kuwa ni kati ya Wema Sepetu na Mh.Freeman Mbowe; Bonyeza hapa chini kusikiliza majibu ya Wema Sepetu; Bonyeza hapa chini kusikiliza majibu ya Mh.Freeman Mbowe; VYANZO: Jamii Forums,                   YouTube.com,                   Perfect255.com.                   

RAPA SNOOP DOGG AMETHIBITISHA MIPANGO YA KUHAMIA UGANDA.

Msanii wa muziki wa Hip Hop wa Marekani, Calvin Cordozar Broadus.Jr. maarufu kama Snoop Dogg amethibitisha kuwa anataka kuhamia Uganda baada ya rais wa Marekani, Donald Trump kudaiwa kuziita nchi za Afrika 'Shimo la Choo' . Snoop Doggy Dogg pia ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki, mtangazaji katika televisheni, na mwigizaji wa filamu ambaye alianza kupata umaarufu mkubwa katika muziki mwaka 1992 wakati alipogunduliwa na mtayarishaji Dr.Dre, na kushiriki katika nyimbo za Dr.Dre kama "Deep Cover", na kisha kwenye albamu ya kwanza ya Dr.Dre, ' The Chronic' . Kwa sasa tayari ameshauza albamu zaidi ya milioni 23 nchini Marekani na albamu milioni 35 duniani kote. Mmarekani huyo mweusi mwenye miaka 46 wa ambaye anajulikana kwa nyimbo zake za maarufu kama; The next episode, Drop it like it’s hot, beautiful, Lay low,  nk Juzi alirekodi kipande cha video na kukisambaza akisema kuwa anataka kuhamia chini Uganda. Tazama V...