Dar es salaam:
Serikali ya Tanzania ,Ijumaa, Septemba 15, ilikanusha taarifa kwamba Tanzania imekiuka vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa dhidi Korea ya Kaskazini.
Ripoti ya wiki iliyopita ilisema kuwa Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi kadhaa za Kiafrika zinazochunguzwa na Umoja wa Mataifa kwa kukiuka vikwazo vilivyowekwa katika nchi hiyo ya bara la Asia.
Lakini katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Dk. Augustine Mahiga, alisema makubaliano ya Tanzania na Korea ya Kaskazini yalikoma mara baada ya vikwazo kuwekwa.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa awali kulikuwa na mikataba na Korea ya Kaskazini katika mikataba ya kidiplomasia, kisiasa, biashara na kijeshi.
"Tanzania imetajwa kua kati ya nchi 11 ambazo zimekiuka vikwazo na kuendelea kushirikiana na Korea Kaskazini," alisema akiongeza:
"Hiyo haiko hivyo kwasababu mara tu baada ya Tanzania kutajwa kwa kuruhusu meli za Korea ya Kaskazini kutumia bendera za Tanzania, tuliomba msaada kutoka kwa mamlaka ya usafiri wa majini ya Kimataifa ambayo ilisaidia kuzipata meli hizo na kuzifutia usajili na kutuma ripoti kwa Umoja wa mataifa."
"Pia Tanzania ilikuwa na makubaliano na Korea ya Kaskazini juu ya kuboresha viungo vya usalama lakini makubaliano yalisimamishwa mwaka 2014 baada ya Tanzania kuombwa kufanya hivyo."
"Kwa hakika tulipaswa kuimaliza taratibu sababu tayari tulikua kwenye mikataba nao, lakini hatukuongeza mikataba mipya nao," alisisitiza.
Aliongeza kuwa Tanzania iliendelea kuwa na majukumu ya mkataba na Korea ya Kaskazini juu ya vifaa vya kijeshi ambavyo Tanzania ilikuwa inakamilisha malipo yake licha ya kuwa nchi hizo zimeacha ushirika.
Alisema kuwa siku ya Jumamosi Septemba 16, angekuwa akienda New York kwa Mkutano Mkuu ambapo anatarajiwa kukutana na wanachama watano wa kudumu wa Umoja wa Mataifa ili kuwahakikishia kuwa Tanzania imeacha uhusiano na Korea Kaskazini.
Hata hivyo alisema kuwa atafanya wazi wazi kwa Tanzania kuwa haikubaliki uamuzi wa Korea ya Kaskazini kuendelea kuzalisha silaha za mahangamizi na kwamba wito wa mazungumzo ya amani kukomesha uadui-sio vitisho vya vinavyo endelea.
CHANZO:
thecitizen.co.tz
Comments
Post a Comment