MRS.GRACE MUGABE. Picha na buzzsouthafrica.com |
JOHANNESBURG:
Mke wa raisi wa Zimbabwe, Grace Mugabe, amekataa madai ya kumshambulia mwanamitindo wa Afrika Kusini
Gabriella Engels na waya wa umeme katika chumba cha hoteli jijini Johannesburg mwezi uliopita, akisema kwamba msichana huyo alikua hajielewi na amelewa na alimshambulia kwa kisu.
Taarifa hiyo ilisema Grace Mugabe, mwenye umri wa miaka 52, na mgombea kuchukua nafasi ya mume wake mwenye umri wa miaka 93 kama rais wa Zimbabwe, alikuwa anafikiri juu ya kufungua mashtaka ya jaribio la mauaji dhidi ya Engels.
Kwa mujibu wa Engels, Mama Mugabe aliyekasirika aliingia ndani ya chumba ambako yeye na marafiki zake wawili walikua wakisubiri kukutana na Chatunga Mugabe tarehe 13 Agosti na kuanza kumshambulia kwa waya wa umeme.
Picha zilizochukuliwa na mama yake baada ya tukio hilo zilionesha majeraha katika paji la uso na kichwa cha Engels. Pia alikuwa na michubuko katika mapaja yake.
Katika madai yake, Mama Mugabe alikataa madai ya Engels na kudai alikuwa ameshambuliwa baada ya kwenda kuwasaidia wanawe waliokua kwenye matatizo na mwanamke mlevi.
"Alikuwa na wasiwasi juu yao na akaenda kuwaona kwenye hoteli zao," ilisema taarifa hiyo. "Baada ya kuwasili, Bibi Engels, ambaye alikuwa amekwisha kunywa na kulewa, alishambulia Mama Mugabe kwa kisu baada ya kuambiwa aondoke hotelini."
"Walinzi walikua hawana uamuzi mwingine zaidi ya kumtoa Engels kutoka katika chumba cha hoteli hiyo"
ripoti iliendelea.
Taarifa hiyo pia imesema kuwa Engels alikuwa katika vita na wanawake wengine katika klabu ya usiku ya Taboo ya Johannesburg usiku uliopita na ilipendekeza kwamba hiyo ndio inaweza kuwa sababu ya majeraha yake.
AfriForum, kikundi cha kiraia cha Kiafrika kinachofanya kwa niaba ya Engels, kilikanusha mashtaka yote.
"Gabriella hakuwahi kushambulia Grace Mugabe kwa njia yoyote na hakushiriki katika vita huko Taboo," AfriForum alisema.
"Ni wazi kwamba Grace Mugabe anajaribu kutoroka majukumu kwa tabia yake mwenyewe ya ukatili kwa kutumia uongo kwa uongo wa kumwonyesha yule aliyeathirika katika kesi hii kama mhalifu."
Afrika Kusini ilitoa kinga ya kidiplomasia kwa Grace Mugabe, ikiruhusu kuepuka mashtaka ya haraka kwa shambulio hilo, ingawa Engels na AfriForum wameshindua uamuzi huo, wakisema Mama Mugabe hakuwa Afrika Kusini kwa shughuli rasmi.
Pia walisema kuwa shambulio lilikuwa ni "uhalifu mkubwa" ambao haukufunikwa na sheria za kinga za kidiplomasia.
Uamuzi wa kuruhusu Grace Mugabe kurudi nyumbani umesababisha mvutano nchini Afrika Kusini kati ya serikari na vyama vya upinzani na kupelekea chama cha Democratic Alliance kwenda kwenda mahakamani kupinga.
CHANZO:
ewn.co.za
Comments
Post a Comment