Ndege kubwa kuliko zote duniani inasemekana kuwa katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuanza safari zake.
Ndege hiyo inayoitwa Stratolaunch yenye injini sita aina turbofan zenye uzito wa kilo 40000 (tani 4) kila moja.
Utengenezaji wa ndege hiyo ni maono ya mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft, ambaye anataka ndege hiyo ndio iwe chombo cha usafiri kikubwa zaidi angani ,chenye kasi zaidi na gharama nafuu kukiendesha kulinganisha na za teknolojia zilizopo sasa.
Mabawa ya ndege hiyo ni marefu kuliko uwanja wa mpira wa miguu ambapo kama ukiiweka katikati ya uwanja wa mpira, mabawa yake yatazidi kwa kwa futi 12.5 (mita 3.8) nyuma ya kila goli.
Tazama kipande hiki cha Video:
CHANZO:
Comments
Post a Comment